MMOJ wa maafisa wakuu wa Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Dk. Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu katika tume hiyo chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi mpya wa urais kufanyika nchini humo.
Dk. Akombe ametuma taarifa kutoka mjini New York anakoishi ambapo alikuwa akiufanyia kazi Umoja wa Mataifa kabla ya kujiunga na tume ya IEBC.
Katika taarifa, Dk. Akombe alisema kuwa merejeleo ya uchaguzi utakaofanyika hayaafikii matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki.
"Uamuzi wangu wa kuondoka IEBC utawasikitisha baadhi yenu, lakini si kwa sababu nilikosa kujaribu. Nilijaribu kadiri ya uwezo wangu ukizingatia hali na mazingira yaliyopo.
Wakati mwingine, unalazimika kusalimu amri na kuondoka, hasa wakati maisha ya watu yamo hatarini," amesema kwenye taarifa hiyo.
"Tume sasa imekuwa kama sehemu ya mzozo wa sasa. Tume imo matatani."
"Imekuwa vigumu kuendelea na mikutano ya tume ambapo Makamishna kila wakati wanalazimika kupiga kura kufanya maamuzi kwa kufuata msimamo wao badala ya kuangazia uzito wa jambo linalojadiliwa.
"Imekuwa vigumu kutokea kwenye televisheni kutetea misimamo ambayo natofautiana nayo kwa sababu ya kuwajibika kwa pamoja.
"Nimefikia uamuzi kwamba siwezi tena kutoa mchango wa maana kwa Tume na kwa taifa langu kama Kamishna."
Dk. Akombe alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la maafisa waliokwenda Dubai kuchunguza uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura.
Dk. Akombe alizuru Nyanza na maeneo ya Magharibi, ambayo ni ngome ya upinzani, wiki iliopita huku tume hiyo ikijaribu kuwafunza maafisa watakaosimamia uchaguzi huo.
Wakuu wa IEBC
Mwenyekiti: Wafula Chebukati
Naibu Mwenyekiti: Consolata Nkatha Maina
Makamishna:
- Boya Molu
- Paul Kibiwott Kurgat
- Abdi Guliye
- Margaret Wanjala Mwachanya
Afisa Mkuu Mtendaji/Katibu:
Post a Comment