Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WALIMU SIKONGE WAIANGUKIA SERIKALI KUWALIPA MADAI YAO.

WALIMU wilayani Sikonge wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kulipa madai ya muda mrefu kwani yamekuwa yakipunguza ari ya utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani Sikonge Perez Kuduhula katika mkutano uliowakutanisha walimu hao kwa lengo la kutathmini utendaji wao wa kazi pamoja na  kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili

Alisema kuwa baadhi ya walimu walishapandishwa madaraja lakini wamekuwa wakiendelea kupata mshahara ule ule wa kabla hajapandishwa.

Kuduhula aliongeza kuwa wapo wengine wamekuwa wakidai gharama za masomo , nauli na gharama za matibabu jambo ambalo linawatia hadi sasa hawajatimiziwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Simon Ngatunga aliwataka walimu hao kuwa wavumilivu kwani serikali inafanya jitihada za kulipa madai yao.

Alisema kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kulipa madai hayo ya walimu kadiri itakavyokuwa ikipokea  fedha .

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa pamoja na changamoto hizo zinazowakabili walimu amewataka walimu kuendelea kujituma ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Alisema kuwa Serikali inaendelea kushughulikia matatizo yao ya ya wale watumishi wengine ni vema wakawa na subira kwani ilikuwa katika zoezi zito la kuhakiki wafanyakazi hewa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora Mwanri ametoa wiki mbili kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya, Mji na Manispaa pamoja na Maafisa elimu wilaya kukaa na Wazazi na Walezi kupanga mipango ya kutekeleza utoaji wachakula kwa wanafunzi kwa shule ambazo hazijaanza kutekeleza mpanga huo.

Alisema kuwa Kiongozi yoyote mwenye dhamana atakayeshindwa kutekeleza jukumu hilo hatasita kumwajibisha kwani ukosefu wa chakula shule hasa kwa wale wanafunzi wanaoishi mbalimbali na shule umekuwa ukisababisha utoro na ufaulu mbaya.


Mwanri alisema kuwa mwanafunzi hawezi kumsikiliza vizuri mwalimu kama anasumbuliwa na njaa na wakati mwingine anatoroka shule pindi anapokuwa na njaa.

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget