Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Diwani Kumbilamoto aeleza sababu ya Zahanati Vingunguti kupatiwa nyota

Image result for naibu Meya ilala
Naibu Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto
NA MWANDISHI WETU, Dar

NAIBU  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto ameeleza sababu zilizopelekea Zahanati ya Vingunguti kufuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali kupitia wakaguzi wake (TRN) na imekuwa miongoni mwa Zahanati tano zilizofuzu.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti  wa Kamati ya Zahanati Ibrahim Aeshi Nduze, Naibu Meya Kumbilamoto ameeleza kuwa hali ya mara ya kwanza katika zahanati hiyo haikuwa sawia  lakini kwa jitihada zake na kushirikiana na Halmashauri na Serikali alifanikiwa kufanya mambo mbalimbali katika maboresho ya zahanati hiyo na hatimae imefanikiwa kupewa hadhi ya nyota nne.

Aliyataja mambo yaliyoweza kuyafanya katika Zahanati hiyo kuwa ni Ununuzi wa Gari ya Wagonjwa (Ambulance), mashine ya kufulia,Jenereta, choo kwa kinamama wanaojifungua, utanuzi wa maabara, ufungaji wa feni nne, mashine tatu za kupimia uzito kwa watoto,kipimo cha presha na kiti cha kubebea wagonjwa.

Zahanati nyingine zilizoweza kupandishwa hadhi katika Halmashauri hiyo  ni  Tabata, Mongolandege, Kinyerezi na Kadilugambwa.

Taarifa kutoka kamati ya Zahanati imeeleza kuwa mwanzo ilikua na nyota mbili ambapo zahanati nyingine zilikua na nyota tatu hivyo vingunguti imepanda nyota mbili.

Kamati hiyo imewashukuru wananchi kwa mawazo, maoni, na changamoto walizozitoa ambazo zimefanyiwa kazi na kuiwezesha  kupata nyota mbili za ziada.

Katika hatua nyingine kamati imemshukuru pia Diwani Kumbilamoto kwa kuwaongoza, kuwashauri, na kutoa mchango wa hali na mali ii kufikia malengo.



Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget