Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Mbunge CCM alivaa jeshi la Polisi Nzega

Hussein Mohammed Bashe
MBUNGE  wa Jimbo la Nzega kwa tiketi ya (CCM) Hussein Mohammed Bashe amefunguka na kusema zaidi ya asilimia 60 ya wakazi wa kijiji cha Undomo kilichopo Kata ya Uchama Nzega wamehama makazi yao kutokana na kamata kamata inayofanya na jeshi la polisi.

Bashe amesema hayo baada ya jana kufanikiwa kuzitembelea familia tano ambazo zimeathirika kutokana na imani za kishirikina ambapo kina mama watano walipigwa na kuchomwa moto na wanakijiji wakituhumiwa kuwa ni wachawi, kufuatia jambo hilo jeshi la polisi liliweza kukamata watu zaidi ya 60 na kuligeuza tukio hilo kama njia ya kujipatia kipato jambo ambalo Mbunge anasema halikubaliki.

"Kina mama watano walipigwa na kuchomwa moto kwa kuwa walituhumiwa kuwa ni wachawi, jeshi la polisi lilikamata watu zaidi ya 60 na uchunguzi unaendelea, jambo jingine ambalo limejitokeza wakazi zaidi ya asilimia 60 wamehama na kufunga nyumba zao kwakua jeshi la polisi limegeuza tukio hilo mradi na kila mtu ambae anakipato hukamatwa na kutakiwa atoe rushwa ama asipotoa anaunganishwa katika kesi jambo hili nimelifikisha kwa mamlaka husika" alisema Bashe.

Mbunge Hussein Bashe akiwa na familia ya Katekista ambae mke wake alichomwa moto na watu wasiokua na utu wala ubinadamu katika kijiji hicho.

Aidha Mbunge Bashe amesema kuwa ofisi yake itashirikiana na jeshi la polisi ili wale waliohusika kweli kwenye tukio hilo waadhibiwe ila wale ambao hawahusiki na wamekamatwa wasigeuzwe chanzo cha mapato kwa askari wa polisi na jeshi hilo.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget