Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

USHAHIDI: Daktari ataja magonjwa mengine ya Kanumba

Marehemu Steven Kanumba
MBELE  ya Jaji Sam Rumanyika leo Oktoba 25, 2017 katika mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam, imemaliza kusikiliza ushahidi wa kesi namba 125/2012 inayomuhusu Msanii Elizabeth Michael maarufu kama 'Lulu' ya kumuua mpenzi wake Steven Kanumba bila kukusudia, ambapo kesho Oktoba 26 Mahakama hiyo itasikiliza maoni ya Baraza la wazee wa mahakama sambamba na kupanga tarehe ya hukumu.

Kwamujibu wa maelezo ya shahidi namba 2  na wa mwisho kwa upande wa mshitakiwa, aliyefahamika kama Josephine Mshumbus yaliyosomwa kwaniaba yake na Staff Sajenti wa polisi Detective E103 Aitwaye Nyangea, aliyotoa 23/04/2012, ameeleza kuwa yeye alimfahamu Marehemu Steven Kanumba Kama Mgonjwa wake katika kituo chake cha tiba mbadala cha Precious Clinic kilichokuwepo karibu na Jengo la Mawasiliano Jijini Dar es sala.

 "Steven Kanumba alikuwa ana matatizo ya sumu mwilini na alikuwa anakuja kwenye kituo changu cha Kliniki Ambapo alikuwa akifanya vipimo vya mwili mzima na aligundulika kuwa na tatizo la Mafuta (Cholestrol), tatizo la Moyo, Upungufu wa Hewa ya Oksijeni kwenye Ubongo ambayo yalimsababishia maumivu makali.

Hata hivyo niligundua kuwa wakati akiendelea na tiba alikuwa akifanya mazoezi ya kutanua misuli, nilimkataza mara moja kwakuwa angeweza kupoteza maisha au Kupooza baadhi ya sehemu za mwili wake.

Kuna siku alikuja kunilalamikia kuhusu maumivu makali anayopata kwenye Moyo, lakini kulingana na wingi wa wateja sikuweza kumuhudumia lakini tulipanga kuonana siku nyingine lakini haikuwezekana tena" Maelezo ya Shahidi yameeleza.

Upande wa Mstakiwa uliongozwa na Wakili msomi Peter Kibatala, Huku Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Faraja George.

Upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi Nne, na Upande wa Mstakiwa uliwasilisha mashahidi Wawili. 
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget