Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

NMB YATOA WITO KWA WATEJA WAKE KUWAFICHUA WATUMISHI WA BENKI HIYO WANAOMBA RUSHWA

Na Tiganya Vincent RS- TABORA
BENKI ya NMB Kanda ya Magharibi imewataka wateja wake kuwafichua watumishi wake ambao sio waadilifu wenye kuonekana kuwa na tabia mbaya ikiwemo kuomba rushwa wakati wanapokuwa wanawahudumia.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Benki ya NMB Leon Ngowi wakati akifunga semina ya siku ya Jukwaa la Biashara la NMB (NMB Business Club) kwa wajasirimali 200 kutoka wilayani Tabora.
Alisema kuwa uongozi wa Benki hiyo hauko tayari kumvumilia mtumishi wake atakayeripotiwa kuwa anamchelewesha kutoa huduma kwa mteja ikiwa ni mbinu ya kutaka apewe chochote ndio amsaidie.
Ngowi alisema kuwa kila mtumishi wa Benki hiyo ni lazima aridhike na kipato anacholipwa na pia atambue kuwa wateja ndio wanawafanya wao kuendelea kuwepo kazini.
Alisema kuwa haifurahishi kumfukuza mtu , lakini endapo mtumishi yoyote atabainika kukiuka maadili ya kazi yake hakuna njia nyingine bali ni kumfukuza.
Ngowi aliongeza kuwa kabla ya kumchukulia hatua mtumishi ambaye ataripotiwa kuwa anakiuka maadili ,taratibu na sheria za kazi zake , uchunguzi wa kina unafanyika ili kuepuka kumwonea mtu wakati wa uchukuaji hatua.
Alitoa wito kwa Mawakala na Wateja wa Benki hiyo popote nchini wanapoona mtumishi anakataa kutoa huduma au wakati mwingine anachelewesha kutoa huduma ili apatiwe chochote watoe taarifa ili wahusika wachukuliwe hatua kwa ajili ya kulinda heshima kubwa ya Benki hiyo.
Kwa upande wa Makalawa wa Benki hiyo wameomba muda wa kuanza kulipa mikopo uongezwe ili walau waanze kulipa miezi mitatu baada ya kuchukua fedha kutoka Benki.
Walisema kuwa hatua hiyo itawasaidia kujipanga vizuri kwani wanapopata fedha wakati mwingine uwachukua mwezi mmoja baada ya kupata fedha hiyo ili kuanza biashara.
Akijibu hoja hiyo Meneja Mikopo wa Benki hiyo kutoka Makao Makuu Stephen Godwin Manji alisema kuwa sio biashara zote zinahitaji mhusika kukaa muda mrefu ndio aanze kulipa fedha.
Alisema kuwa Benki hiyo inaoutaratibu mzuri ambapo inazingatia kuwa mhusika anafanyabiashara gani na bidhaa zake anazitoa wapi wakati wa taratibu za kuanza malipo.
Aidha Meneja huyo alisema kuwa muda sio mrefu Wateja wa Benki hiyo wataweza kupata mkopo wa kufikia milioni 50 utakaokuwa umeidhinishwa na Meneja wa Tawi lake na sio Makao Makuu kama ilivyokuwa zamani.
Alisema kuwa mchakato unaendelea vizuri mara utakapokuwa tayari wateja wao wataanza kupata mkopo wa kiasi hicho baada ya idhini ya Meneja wa Tawi lao. 

Mafunzo hayo ni mwendelezo wa Benki hiyo kuwaelimisha Mawakala wake juu ya mambo mbalimbali ikiwemo umuhimu wa ulipaji kodi na utunzaji mzuri wa kumbukumbu za biashara zao kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuwa na biashara endelevu.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget