Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Dk. Mashinji: "Ili tupate Katiba mpya tuikate CCM"

Image result for katibu mkuu chadema
Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Vicent Mashinji
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk Vicent Mashinji amewataka wananchi kukikataa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 iliwaweze kupata katiba mpya

Dk. Mashinji amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema njia pekee ya kuweza kupata katiba mpya ni kuikataa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka
2020

"Mh. Rais alishaongea kuwa katiba si ajenda yake na kwenye kampeni zake hakuwahi kuongelea na Ilani ya uchaguzi ya wenzetu imeongelea kuwa watakamilisha hiyo katiba sasa kuna hatua

mbalimbali sisi tunapaswa kuzichukua kama wananchi, moja ili tuweze kupata katiba cha kwanza ni kukikataa Chama Cha Mapinduzi hilo ndilo jambo kubwa tunatakiwa kulifanya, hivyo ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 hatuichagui kuongoza serikali" alisema Dk Mashinji

Aidha Katibu huyo wa CHADEMA amedai kuwa katika bunge hili la sasa kuna hoja binafsi ambayo imelenga kuelezea maboresho ya tume ya uchaguzi nchini (NEC) ikiwa ni

katika hatua za kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 wanapata haki katika uchaguzi huo mkuu.


"Katika bunge hili kutakuwa na hoja binafsi ambayo itawasilishwa na Mh. Silinde na huu utakuwa mwanzo wa mabadiliko katika taifa hili najua kuna wananchi wengi sana wangependa tudai katiba yetu kwa nguvu, kwa hoja za nguvu na si nguvu za hoja hizi ndiyo njia mbili tulizonazo ambazo tunaziweka kwenye mezania, hivyo kwanza tunatumia njia za kidemokrasia na kidoplomasia endapo njia hizi zote hazitazaa matunda ambayo wananchi wanahitaji tutawaomba wao wachukue uongozi katika jambo hili" alimalizia Mashinji
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget