Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

RC TABORA AZUIA MALIPO YA ZAIDI MILIONI 300 BAADA YA MIKATABA MWILI YA UJENZI WA MIRADI SIKONGE KUKIUKWA .

Image result for mkuu wa mkoa wa Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
Na Tiganya Vincent,Sikonge


SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kutolipa malipo ya kiasi cha zaidi ya milioni 300 kwa ajili ya miradi miwili ya maendeleo ambayo imebainika kuwa na kasoro mbalimbali.

Agizo hilo limetolewa jana mjini Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kikungi Kata ya Chabutwa na ujenzi wa barabara ya lami mjini Sikonge.

Alisema katika mradi wa Zahanati  maelezo Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge yanaonyesha kuwa mjenzi wa Zahanati huo amekiuka makubaliano ya mpango wa ujenzi na vifaa vitakavyotumika katika (BOQ).

Mwanri alisema kuwa mjenzi wa Zahanati hiyo amekuwa akitumia vifaa zaidi au pungufu na wakati mwingine ametumia vifaa katika ujenzi wa majengo ya ZAhanati hiyo ambavyo havikuonyeshwa katika BOQ bila makubaliano na Halmashauri hiyo.

Kwa mujibu wa makubaliano mradi huo wa Zahanati unapaswa kugharimu shilingi milioni 170 ikiwa ni gharama za vifaa shilingi milioni 130 na gharama za mjenzi milioni 40 lakini kwa sababu ya mjenzi wake kutofuata maelezo ya BOQ zinaweza kuzidi.

Katika mradi wa pili ambao ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa urefu kilometa moja kwa gharama za shilingi milioni 220.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema mradi huo unaonekana kujengwa chini ya kiwango na muda ambao mkandarasi alipaswa ameameashamaliza umeshapita.

Kufuatia kasoro hizo katika miradi hiyo miwili Mkuu huyo wa Mkoa amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Sikonge kutoidhinisha malipo ambayo yalikuwa hayajafanyika kwa mjenzi wa Zahanati ya Kikungi ya shilingi milioni 170 na yale yaliyokuwa yamebaki ya zaidi shilingi milioni 70 zilizokuwa zimebaki kwa mradi wa barabara.

Alisema kuwa wajenzi wote wa miradi hiyo watalipwa baada ya timu ya wataalamu kutoka Mkaguzi wa Hesabu Serikali za Mitaa  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Wakala wa Barabara Tanzania mkoa wa Tabora, Taasisi ya Kupambana na kudhibiti Rushwa(PCCB) na Wakala wa Majengo Tanzania(TBA).

Mwanri alisema timu hiyo inalenga kutafuta ukweli kama taratibu za kutoa zabuni kwa wajenzi zilifuatwa na ikiwa vifaa vilivyotumika vinalingana na thamani halisi ya fedha na makubaliano katika BOQ.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sikonge Simon Ngatunga alisema kuwa alisema katika mradi wa Zahanati mjenzi aliamua kutumia baadhi ya vifaa hata ambavyo havimo katika BOQ bila hata kuijulisha Ofisi yake.

Alisema kuwa katika mradi wa barabara licha ya kutokwisha unaonyesha kuwa uko chini ya kiwango na kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuunda timu ya wataalamu kuchunguza miradi hiyo ili waone kama iko katika kiwango.

Ngatunga alisisitiza kuwa hawezi kulipa hadi hapo timu ya wataalamu hapo itakapomuhakikishia kuwa taratibu zote zimezingatiwa.



Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget