Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Tamko la waziri Kairuki kuhusu nyongeza ya mishahara

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki 
 NA MWANDISHI WETU Dodoma

SERIKALI  imesema bado haijapandisha mishahara lakini hilo litafanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema Serikali haikupandisha mishahara kutokana na sakata la watumishi hewa na vyeti feki ambalo mchakato wake sasa umekwisha.

“Tayari Serikali imeshatenga Sh600 bilioni kwa ajili ya kuanza kupandisha madaraja wafanyakazi wote ambao wanastahili,” amesema.

Kairuki alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Susan Masele  ambaye pia ametaka kujua kuhusu idadi ya vibali vya ajira vilivyotolewa na Serikali.

Waziri amesema Serikali imeshasaini vibali 10,000 kwa ajili ya kutoa ajira na vingine 4,000 viko mbioni kusainiwa.

Amesema sehemu itakayoangaliwa kwanza katika kuajiri ni nafasi za walimu na idara ya afya ambazo ndizo zilionekana kuathiriwa zaidi na vyeti feki.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget