Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Marekani yailaumu Korea Kaskazini kwa kuomba vita

Haley amesema teknolojia ya Korea ya Kaskazini kwenye mabomu ya nyukilia ni ya hatari na haina mfano
Image captionHaley amesema teknolojia ya Korea ya Kaskazini kwenye mabomu ya nyukilia ni ya hatari na haina mfano
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa ameilaumu Korea ya Kaskazini kwa kulazimisha vita kutokana na majaribio yake ya makombora ya mara kwa mara.
Nikki Haley ametaka kuwepo kwa muda wa dharura wa Baraza la Umoja wa Mataifa utakao jibu majaribio hayo kwa hatua kali.
"Vita sio kitu ambacho Marekani ingetaka," alisema. "Hatutaki vita kwa sasa lakini uvumilivu wa nchi yetu hautuzuii."
Baadae, kupitia mazungumzo ya simu na Rais Trump, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema atahimiza kuwepo kwa vikwazo vikali kutoka umoja wa nchi za ulaya dhidi ya Pyongyang.
Hata hivyo, China imesisitiza wito wake wa kutaka pande zote zirudi katika meza ya mazungumzo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa mara ya mwisho liliweka vikwazo kwa Korea Kaskazini juu ya bidhaa zake mwezi Agosti
Image captionBaraza la usalama la umoja wa mataifa mara ya mwisho liliweka vikwazo kwa Korea Kaskazini juu ya bidhaa zake mwezi Agosti
Ripoti zinasema kuwa Korea Kaskazini inajiandaa kwa majiribio mengie ya makombora.
Siku ya Jumapili ilifanya jaribio la bomu la chini ya ardhi lililoaminika kuwa na nguvu ya kati ya kilotani 20 na 120.
Kifaa hicho hicho kinaweza kuwa na nguvu mara tatu zaidi ya bomu lililotumiwa kuharibu mji wa Hiroshima mwaka 1945.
China haitaki kuwepo nchi yenye silaha za nyuklia ya Korea Kaskazini na mara kwa mara imeeleza msimamo wake kwa nchi hiyo.
Lakini pia haitaki kuona utawala wa Korea Kaskazini ukiondolewa madarakani. Hii itasababisha mamilioni ya wakimbizi kukimbia kwenda China na kuchangia kuungana kwa Korea ambayo itakuwa chini ya ushawishi wa Marekani.
chanzo BBC News
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget