Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Maagizo ya TFF kwa makocha wa ligi kuu wasiokidhi vigezo


TFF kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu Wilfred Kidao, imetoa maagizo pamoja na maangalizo kwa makocha wanaoongoza timu za ligi kuu Tanzania bara.

Kuna makocha ambao huwakimbia waandishi wanapotaka kufanya nao mahojiano baada ya mechi kumalizika. Pia kumekuwa na utaratibu mgumu wa kufanya mahojiano na makocha siku kadhaa kabla ya mechi ili kuzungumzia kiufundi kuelekea mchezo husika.

“Nitatoa maelekezo waalimu wote wawe wanaongea siku kadhaa kabla ya mechi na baada ya mechi. Kuna kanuni zinalazimisha siku kadhaa kabla ya mechi wazungumze, wasipofanya hivyo wanapigwa faini,” – Kidao.

Kwa upande wa makocha ambao wanasoma kisha kuvifungia ndani vyeti vyao bila kufanya kazi ya kufundisha soka, Kidao amewagusa pia.

“Hakuna kocha ambaye atapewa course ya juu bila kuona shughuli anazozifanya, lengo ni kuhakikisha tunakuwa na makocha bora tofauti na sasa hivi tuna namba kubwa ya makocha lakini hawana ubora” – Kidao.

Kwa wale makocha ambao hawajakidhi vigezo vya kuwa kwenye mabenchi ya ufundi ya timu za ligi kuu nao siku zao zinahesabika.

“Kila timu inatakiwa kuwa na kocha mkuu ambaye leseni yake ni kuanzi Daraja B iliyotolewa na CAF na kuendelea, kocha msaidizi awe na leseni ya kuanzia Daraja C kwenda juu. Kama kuna timu ya ligi kuu ina kocha mkuu ambaye hana sifa hizo hatua zitachukuliwa.”

Kuna tetesi kwamba kuna timu ya ligi kuu inamtumia kocha ambaye leseni yake ni Daraja C na anasimama kwenye timu hiyo kama kocha mkuu.

“Timu inaweza kumtumia kocha mwenye leseni Daraja C bila ya kuwa na kocha mkuu, lakini kocha huyo anakuwa amesajiliwa bodi ya ligi kama kocha msaidizi. Na kuna muda wa kuwa na kocha msaidizi bila kocha mkuu baada ya hapo timu itaadhibiwa kwa kukosa kuwa na kocha mkuu mwenye vigezo.”
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget