Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Mwita aitumbua kampuni ya ukusanyaji ushuru wa maegesho ya magari

NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amesitisha  mkataba na Kampuni ya Mwamkinga Auction Mart and Brokers iliyokuwa ikifanya kazi ya kudhibiti uegeshaji wa magari katika maeneo yasiyo rasmi kwa Halmashauri ya Temeke na Kigamboni.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mapema leo asubuhi Meya Mwita amesema kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na kampuni hiyo kufanya kazi kwakutozingatia matakwa ya mkataba na hivyo kuanzisha migogoro isiyo ya lazima baina ya halmashauri ya jiji na Wananchi.

Meya mwita amefafanua kuwa jiji liliingia mkabata na kampuni hiyo Aprili mwaka huu kwa lengo la kufanya kazi hiyo ambapo mkataba huo ulielekeza kufanya kazi kwa weledi mkubwa, kuzingatia sheria, miongozo ,maelekezo, kanuni na taratibu zilizopangiwa bila kusababisha bughudha, uonevu, kero na usumbufu kwa wananchi jambo ambalo halikufanyika.

 “ Hii kampuni imekuwa ikilalamikiwa mno na wananchi, inawasumbua, na sisi kuwapa tenda hii sio kwa ajili ya kuwanyanyasa, kuwasumbua ila ni kufanya kazi kwa weledi”

 Nakuongeza kuwa” tumefuatilia kwa karibu sana utendaji kazi wao, kutokana na malalamiko ambayo yalikuwa yanatolewa na wananchi, tukajiridhisha, kwa ushahidi uliojitosheleza, hawawezi kunyanyasa watu na mimi kama meya wa jiji hili nikawaachia, hili haliwezekani” amesisitiza Meya Mwita.

Hata hivyo ameeleza kuwa kampuni hiyo inapaswa kuondoka mara moja kwenye maeneo iliyopangiwa kufanya kazi hiyo na kuhakikisha kwamba katika kuanzia tarehe ambayo mkataba huo umesitishwa iwe imekabidhi mashine zote za kukusanyia mapato kwa halmashauri zikiwa kwenye hali salama.

Aidha Meya Mwita amesisitiza kuwa hata sita kuzichukulia hatua kampuni nyingine ambazo zimepewa tenda hiyo na kuzionya kuwa iwapo wanatabia hiyo waache mara moja kwani kazi waliyopewa sio ya kusanyanyasa wananchi bali ni kufanya kazi kwa kufuata sheria.


Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget