Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Meya wa jiji la Dar Mwita akutana nakufanya mazungumzo na Meya wa jiji la Xin'an Nchini China

DSC_2252
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye suti nyeusi akiwa na Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya mazungumzo leo alipomtembelea mfisini kwake.
DSC_2256
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisalimiana na Meya wa jiji la Xin’an  Zhu Huan alipomtembelea ofisini kwale leo na kufanya nae mazungumzo.

DSC_2239
Mstahiki Meya wa jiji la Xn’an Nchini China Zhu Huan akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kufaya mazungumzo na mwenyeji wake Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kufanya mazungumzo  mbalimbali.


DSC_2244
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amekutana na kufanya mazungunzo na Meya wa Jiji la Xin’an Nchni China Zhu Huan ofisini kwake Karimjeee.
Katika mazungumzo hayo , Meya Mwita na mgeni wake wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kukuza na kutangaza utalii wa ndani na nje ya Dar es Salaam.
Aidha Meya Mwita amesema jiji la Dar es Salaam lina kila aina ya vivutio vya utalii wa ndani na nje ambavyo vinaweza kuwavutia wageni mbalimbali kutoka nje ya Nchi kufika jijini hapa na kutalii badala ya kwenda  Zanzibar , Kilimanjaro na maeneo mengine.
Ameongeza kuwa anaamini kuwa mazungumzo hayo na mgeni wake yataleta tija na kwamba jiji la Dar es Salaam litapata watalii kutoka sehemu mbalimbali na hivyo kuliwezesha jiji kupata mapato makubwa kupitia vivutio vilivyopo.
“ Tunania ya kulitagaza jiji letu kwenye sekta ya utalii, kutokana na rasilimali za vivutio vilivyopo, ukienda kwenye maeneo mengi ndani ya jiji letu utaona kuwa tunavyo vivutio vyakutosha kabisa ambavyo vikitangazwa kila mmoja atapenda kutalii katika jiji hili” amesema Meya Mwita.
“ Yapo maeneo mengi ambayo watanzania hawayajui, lakini kupitia mpango huu ambao nimekuja nao hivi sasa ninaimani kwamba watu ambao walikuwa wanafika kwenye jiji letu na kupanda ndege kwenda Zanziba ama Arusha na maeneo mengine, sasa watafanya utalii hapa kwetu” amesisitiza.
Meya Mwita ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa , hivi karibuni jiji la Dar es Salaam linaratajia kupokea magari ya utalii ambayo yamenunuliwa kupitia fedha za jiji, ambapo baada ya kufika yatazinduliwa na hivyo kuanza kutangaza utalii wa ndani.
Kwaupande wake Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan amempongeza Meya Mwit kutokana na uendeshaji wake wa jiji, ambapo amesema jiji la Dar es Salaam limepata Meya bora ambaye anaamini kwamba ataleta mabadiliko makubwa ndani jiji hili.
Mbali na pongezi hizo, pia ameahidi kushirikiana nae katika sekta mbalimbali ikiwemo kutangaza utalii wa jijini hapa ili uweze kutambulika katika maeneo mengine Nchini China.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget