Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Wanafunzi 917,072 Darasa la saba kutahiniwa kesho.

Image result for dk msonde
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dk. Chrales Msonde.

NA CHRISTINA MWAGALA, Dar

WANAFUNZI 917,072 wa darasa la saba kutoka shule za Msingi 16,583 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kesho Jumatano na Alhamisi.

Kati ya wanafunzi hao, inadaiwwa kuwa  wavulana ni 432,744 sawa na asilimia 47.19 , huku wasichana wakiwa 484,328 sawa na asilimia 52.81.

Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam mapema leo asubuhi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dk. Charles Msonde amesema kuwa watahiniwa hao watafanya mtihani wa masomo ya Kiswahili, Englishi Language, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya jamii.

Dk. Msonde amesema kati ya watahiniwa  917, 072  waliosajiliwa kufanya mtihani huo, watahiniwa 882,249 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 34,823 watafanya mtihani kwa lugha ya Kingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia.

Amesema kuwa watahiniwa wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani huo ni 94 wakiwemo wavulana 58 na wasichana 36, huku watahiniwa wenye uoni hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa wapo 1,138 ambao pia wavulana ni 586 huku wasichana wakiwa 552.

Dk.Msonde amesisitiza kwamba maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mitihani , fomu maalumu za OMR, zakujibia mtihani na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo katika halmashauri zote hapa nchini.

“ Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla, kwa kuwa hupima uwezo na uelewa wa wanafunzi katika yale yote waliojifunza kwa kipindi cha miaka saba” amesema Dk. Msonde.

Aidha Dk. Msonde ametoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha kuwa taratibu zote za uendeshaji wa mitihani wa Taifa zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba mazingira ya vituo hivyo yapo salama.

“ Baraza pia linatoa wito kwa wasimamizi wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu ,pia wajiepushe na vitendo vya udanganyifu, atakaye bainika hatutasita kumchukulia hatua” amesisitiza Dk. Msonde.

Hata hivyo Dk. Msonde aliwakumbusha wamiliki wa shule kutambua kwamba shule zao ni vituo maalumu vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyikaji wa mitihani.


Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget