Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Mbowe Amshangaa Spika na Waziri Ummy Mwalimu Matibabu ya Tundu Lissu

Mbowe Amshangaa Spika na Waziri Ummy Mwalimu Matibabu ya Tundu LissuMWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amemshangaa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema kuwa Serikali iko tayari kumtibu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu popote duniani.

Mbowe ametoa mshangao huo jana Ijumaa alipokuwa akitoa taarifa kuhusu matibabu ya Lissu yanayoendelea jijini Nairobi. Amesema wakati walipoamua kumpeleka Lissu jijini Nairobi, Waziri Ummy alikuwepo lakini walitaka Lissu apelekwe Muhimbili kwanza na baadaye kama angepata rufaa angepelekwa nchini India.

“Sasa wiki mbili baadaye ndio anatoka Waziri wa Afya anasema Serikali iko tayari kumtibu popote duniani, eh kweli? Mama Ummy Mwalimu anasahau kauli yao wakinieleza mimi pale Dodoma, wamuogope Mungu, walikataa ‘categorically’ pengine walifikiri wao ni miujiza mheshimiwa Lissu kupona na sisi tulisema lazima tumpeleke Nairobi ndiyo mahali tunaona kweli kunawezekana kukaokoa yale maisha,”amesema Mbowe.

“Ilikuwa ni hatari na ni maamuzi yalikuwa magumu sana, watu ambao wana mamlaka, Waziri wa Afya yuko pale, Spika yuko pale nawaambia fanyeni maamuzi tumuokoe huyu mtu wanasema hatuwezi kumpeleka Nairobi, mimi nikasisitiza sisi tunampeleka Nairobi wakasema basi utalipa mwenyewe, nikasema sawa tutalipa wenyewe.”

Pamoja na hayo Mh. Mbowe amesema kwamba Spika wa bunge kupitia wasaidizi wake alimtafuta siku chache zilizopita na kumtaarifu kwamba Serikali inaweza kusaidia matibabu ya Lissu lakini kwa masharti matatu, ikiwa ni wakubali apelekwe India, aandikie barua ya maombi na tatu apeleke taarifa yote kuhusu matibabu ya hospital ya mgonjwa na kwa upade wake alikataa.

Ameongeza "Jana Ummy anasema familia iandike maombi siyo chama maana mimi nilikataa. Wabunge kutibiwa na serikali ni stahiki. Wabunge wengi wametibiwa kwa nyakati tofauti  labda kama ingekuwa anaumwa mtoto wa Lissu na anatibiwa kwa kofia ya baba yake ndio baba yake angeomba. Lakini kuhusu mimi kuandika sitaweza kuandika labda Spika ajiandikie yeye, au familia ya Lissu iandike lakini mimi nimesema kama kiongozi wake wa chama sitaweza.

Hata hivyo Mbowe amesema hiyo ni hali halisi ambayo ameona awaambie Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwashukuru watu mbalimbali waliochangia  matibabu ya Lissu na kuwaomba kuendelea kuchangia matibabu ya Tundu Lissu.

Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget