
Mbali na Manji ambaye ni mfanyabiashara , washitakiwa wengine waliokabidhiwa ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda, Mtunza stoo, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.
Akiwakabidhi watuhimiwa hao, wakili wa serikali mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa washtakiwa hao wamerudishwa mahakamani kama ilivyoamuriwa, baada ya polisi kumaliza kuwahoji.
Baada ya washtakiwa kukabidhiwa wakiwa salama na afya zao nzuri, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itaendelea na utaratibu kama ulivyokuwa awali, ambapo itatajwa September 8/2017.
Jana mchana mahakama hiyo iliruhusu Manji na wenzake kwenda kuhojiwa na Polisi ili kukamilisha upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi.
Post a Comment