Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Wanawake ruhsa kuendesha magari Saudia

Saudi
Image captionWanawake wa Saudi Arabia sasa kuruhusiwa kuendesha gari
MFALME Salman wa Saudi Arabia ametoa idhini ya wanawake kuendesha magari, hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa. Uamuzi huu umefikiwa kutokana na harakati za muda mrefu kwa makundi ya wanawake na haki za bindamu kushinikiza wanawake waruhusiwe kuendesha magari.
Kwa muda mrefu Saudi Arabia imekuwa nchi pekee Duniani kuwazuia wanawake kuendesha magari. Abdallah al-Mouallimi Mwakilishi wa umoja wa mataifa kutoka Saudia ametangaza habari hizi umoja wa huko umoja mataifa.
"Ndugu Mwenyekiti, Mabibi na mabwana. Najua mtapenda kujua jambo hili kwamba dakika chache zilizopita Mfalme amepitisha sharia inayowapa idhini,wanawake nchini Saudia kuendesha magari.Hii ni historia mpya leo kwa jamii ya Saudia,kwa wanaume na wanawake.Na kwa sasa tunaweza kusema kitu angalau.'' Abdallah al-Mouallimi.
Saudia
Image captionWanawake wa Saudia
Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa idara ya Marekani,Bi.Heather Nauert amelezea kupokea kwa furaha tangazo hilo.
"Tuna wanafuraha kusikia jambo hilo,kwamba wanawake wa Saudia sasa wanaruhusiwa kuendesha magari,kwa hapa Marekani tunafurahia jambo hilo,na kuona ni hatua kubwa na mwelekeo mzuri kwa taifa hilo'' Heather Nauert.
Mwanaharakati wa Saudi Arabia aliyewahi wekwa kizuizini kwa siku 73 kutokana na kupinga wanawake kuzuiwa kuendesha magari, ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter akisema 'Thank you God', yaani asante Mungu.
Sheria hii inaanza kufanya kazi mwezi june mwaka ujao, na kwa sasa wizara itatakiwa kuandaa ripoti maalumu kuhusiana na jambo hilo.

Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget