Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Simba yampa Okwi kibarua kizito

Mshambuliaji wa timu ya Simba, Emmanuel Okwi.

BENCHI la ufundi la Simba likiongozwa na kocha wake mkuu, Joseph Omog raia wa Cameroon limempa kazi nyota wao, Emmanuel Okwi kuhakikisha anaibeba timu hiyo katika mchezo wake wa wikiendi hii dhidi ya Azam FC.

Simba na Azam zinatarajiwa kukutana wikiendi hii kwenye pambano la Ligi Kuu Bara ambalo limepangwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Awali mchezo baina ya vikosi hivi viwili ulipangwa kupigwa Agosti 2, mwaka huu kabla ya kupanguliwa kutokana na kuingiliana kwa ratiba ya TFF na Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Kikizungumza na Championi Jumatano, chanzo makini toka ndani ya Simba kimesema kuwa benchi hilo limefikia maamuzi hayo kutokana na muendelezo mzuri wa Okwi katika kufunga mabao ambao ni mzuri kulinganisha na washambuliaji wengine wa timu hiyo.

“Benchi letu limekaa na kuona kwamba ni Okwi pekee ambaye anaweza kutubeba kwenye mchezo huu na Azam kwa kuzipata pointi za wapinzani wetu hao, hivyo kila kitu ameachiwa yeye na atakaporudi nchini toka Uganda, basi atapewa ujumbe huo na mtu maalum wa kumpa wameshaandaliwa.

“Wameamua hivyo kwa sababu yeye ndiye mwenye rekodi nzuri ya kufunga mabao kulinganisha na washambuliaji wengine waliopo hapa, na imani yetu ni kwamba atalitimiza suala hilo kikamilifu kwa sababu ameshazoea kuamua matokeo kwenye michezo mikubwa kama alivyofanya hivi karibuni wakati akiichezea timu yake ya Uganda dhidi ya Misri,” kilisema chanzo hicho.

Championi Jumatano, lilimtafuta kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, ambapo alisema: “Okwi ni mshambuliaji mzuri linapokuja suala la kufunga mabao, tunamuamini kwamba atatubeba tu siyo kwenye mchezo huo bali kwenye kila mechi yetu ya ligi kuu.”
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget