Mbunge viti maalumu achanganywa na agizo la Mwigulu
NA MWANDISHI WETU, Dodoma
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Jesca Kishoa amesema agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba la kuwataka wabunge wanawake wafanye mikutano katika vyama vyao badala ya mikoa wanayotoka ni la kibaguzi na kinyume cha Katiba.
Kishoa amesema hayo baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni alipoomba mwongozo wa Spika kuhusu kauli aliyodai ilitolewa juzi Septemba 3 na Mwigulu.
"Kauli hii inatofautiana na aliyoitoa Machi kwamba, wabunge wa viti maalumu wanaruhusiwa kufanya mikutano katika mkoa na wabunge wa majimbo kwenye majimbo yao tu," amesema.
Hata hivyo, Spika Job Ndugai amemjibu mbunge huyo kwamba, alichomaanisha Mwigulu ni kuwa wabunge wa majimbo wanaruhusiwa kuzungumza na wapiga kura.
“Sasa wapiga kura wenu wapo kwenye mikutano ya hadhara?" amehoji Ndugai.
Post a Comment