Rais wa urusi Vladimir Putin |
Marekani ilisema Jumatatu kuwa itapeleka azimio mpya kwa Umoja wa Mataifa la vikwazo zaidi, kufuatia hatua ya nchi hiyo kulifanyia majaribio bomu la nyuklia siku ya Jumapili.
Bwana Putin pia alisema kuwa hatua za kijeshi inaweza kuleta janga la dunia nzima.
China, mshirika mkuu wa Korea Kaskazini pia nayo imetaka kurejelewa kwa mazungumzo.
Sanctions have been exhausted.Haki miliki ya pichaREUTERS
Putin alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa nchi za Brics ambazo ni (Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini) huko Xiamen nchini China. Licha ya Putin kuishutumu Korea Kaskazini, alisema kuwa vikwazo havitasaidia.
Siku ya Jumatatu mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley, alisema kuwa vikwazo vikali vitasababisha tatizo hilo kutatuliwa kwa njia ya kidiplomasia.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel aliunga mkono pendekezo hilo akisema kuwa vikwazo vya haraka vinahitajika kukabiliana na tabia ya Korea Kaskazini kukiuka maazimio ya kimataifa.
Rais wa Korea Kusini Kim Jong |
Post a Comment