Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WANANCHI WAFURIKA KUPIMA AFYA BURE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

 

Zoezi la Upimaji wa Afya Bure limeanza leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,huku baadhi ya Wananchi wakitoka Mikoani kuja Dar es Salaam kufuata huduma na wengine wakiwahi kwenye Viwanja hivyo tokea saa 10 Alfajiri.

RC Makonda amesema kampeni hiyo ina malengo matatu ambayo ni:

  • Kujengea Wananchi utaratibu wa kupima Afya zao Mara kwa mara hata kama hawaumwi.
  • Kusaidia Wananchi Wanyonge wanaotamani kupima Afya lakini hawana Uwezo wa Fedha kupata fursa ya kupima Afya.
  • Kupunguza vifo vitokanavyo na watu kutokujua historia ya Magonjwa yao hadi pale wanapougua.


Aidha Makonda amesema kila Mwananchi atakaefika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja atapimwa na kupatiwa Matibabu Bure.

Amesema Wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa utaratibu wa kupima Afya Mara kwa Mara na pindi wanapozidiwa na kufikishwa Hospital Ugonjwa unakuwa tayari umekuwa sugu hivyo kupoteza maisha.

Amewapongeza Madaktari na Wauguzi kutoka Hospital za Umma, Jeshi na zile za Binafsi kwa kujitolea kumuunga mkono katika Kampeni hiyo.


Zoezi la upimaji Afya Bure litaendelea Kwenye Viwanja vya Mnazu Mmoja kwa muda wa siku tano kuanzia Asubuhi hadi Jioni.





Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget