Na Tiganya Vincent,Sikonge
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imemwagiza kuwakamata waliokuwa viongozi wa Chama cha Ushirika cha Mibono na wale Tupendane kwa ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za wakulima na vyama hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano ambao ni sehemu ya utekelezaji wa magizo ya viongozi wakuu wa kitaifa waliotembelea mkoa huo na kuwaagiza kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Alisema kuwa viongozi wote wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za vyama na wakulima na wale wakulima wa tumbaku waliotorosha tumbaku katika msimu wa 2013/14 watafutwe popote walipo na kukamatwa ili waweze kufikishwa Mahakamani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria. ni kubainika matumizi mabaya ya fedha za za AMCOS na wengine kula hata
Mwanri alisema kuwa hata kama kuna kiongozi yoyote aliyehusika na ambaye amehama ni vema akarudishwa ili aweze kujibu mashataka yake ya kula fedha za wakulima.
“Nakuagiza DC shirikiane na OCD mkitumia taarifa ya ukaguzi wa vyama vya msingi hivyo fedha za wakulima …kisha muwakamate na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili wapate adhabu inayowastahili.” Alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Ufuatiliaji Fedha za wakulima za Msimu wa 2013/14 Valerian Kaozya akitoa kero yao kwa Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa baadhi ya wakulima wa Mibono AMCOS wapatao 441 wanadai zaidi ya shilingi milioni 966 toka msimu huo.
Alisema kuwa hatua imewatokana na baadhi ya viongozi wa mibono kujichukulia fedha na kufanya malipo bila hata kufuata taratibu na kukuta fedha zao zikiishia katika mifuko yao.
Kaozya aliongeza kuwa ukaguzi uliofanywa na Ofisi ya Halmashauri ya Sikonge ulithibitisha ubadhirifu uliofanywa na viongozi hao kwa kujilipa mamilioni ya fedha na nyingine kulizipa kwa majina hewa jambo lililosababisha wao kukosa fedha zao.
Alisema kuwa wapo pia wakulima 131 walitorosha tumbaku yao na kukiachia Mibono AMCOS deni la zaidi ya milioni 75 ambazo ziliathiri wakulima waliokuwa wamemaliza madeni yao kushindwa kulipwa na NMB.
Kwa upande wa viongozi wa Tupendane AMCOS walituhumiwa kwa kujichukulia milioni zaidi ya 150 mali ya wakulima kwa kutumia hati za kughushi na kuwa sababisha wao kushindwa kulipwa fedha za msimu 2013/14.
Naye Meneja wa NMB Sikonge Stewart Singo akijibu baadhi ya hoja alisema kuwa wakulma wa Mibono AMCOS walishindwa kupata malipo yao kwa kuwa tumbaku iliyouzwa ilikuwa chini ya makisio ya kilo 800,000 walipanga kuuza badala yake waliuza kilo 400,000.
Alisema kuwa hali hiyo ilisababisha Chama hicho kuwa na deni kwa kushindwa kulipa deni walikopeshwa na benki kupitia ushirika wao.
Post a Comment