Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Vicent Mashinji |
Dk. Mashinji amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema njia pekee ya kuweza kupata katiba mpya ni kuikataa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka
2020
"Mh. Rais alishaongea kuwa katiba si ajenda yake na kwenye kampeni zake hakuwahi kuongelea na Ilani ya uchaguzi ya wenzetu imeongelea kuwa watakamilisha hiyo katiba sasa kuna hatua
mbalimbali sisi tunapaswa kuzichukua kama wananchi, moja ili tuweze kupata katiba cha kwanza ni kukikataa Chama Cha Mapinduzi hilo ndilo jambo kubwa tunatakiwa kulifanya, hivyo ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 hatuichagui kuongoza serikali" alisema Dk Mashinji
Aidha Katibu huyo wa CHADEMA amedai kuwa katika bunge hili la sasa kuna hoja binafsi ambayo imelenga kuelezea maboresho ya tume ya uchaguzi nchini (NEC) ikiwa ni
katika hatua za kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 wanapata haki katika uchaguzi huo mkuu.
"Katika bunge hili kutakuwa na hoja binafsi ambayo itawasilishwa na Mh. Silinde na huu utakuwa mwanzo wa mabadiliko katika taifa hili najua kuna wananchi wengi sana wangependa tudai katiba yetu kwa nguvu, kwa hoja za nguvu na si nguvu za hoja hizi ndiyo njia mbili tulizonazo ambazo tunaziweka kwenye mezania, hivyo kwanza tunatumia njia za kidemokrasia na kidoplomasia endapo njia hizi zote hazitazaa matunda ambayo wananchi wanahitaji tutawaomba wao wachukue uongozi katika jambo hili" alimalizia Mashinji
Post a Comment