MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa deni la Tsh 424 trilioni inayoidai Migodi ya Bulyanhulu Gold Mine (BGML) na Pangea Minerals (PML) inayoendeshwa na Acacia limekokotolewa na wataalamu wa kodi waliobobea waliokuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati mbili za kuchunguza makinikia zilizoteuliwa na Rais Magufuli.
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na gazeti la MTANZANIA jana, Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa TRA, Gerald Mwanilwa alisema,
“Deni la Acacia halikuja kibahati mbaya, lilikokotolewa na wataalamu wabobezi wa masuala ya kodi tangu (BGML na PML) walipoanza kukwepa kodi hadi tulipobaini jambo ambalo limesababisha deni kuonekana kubwa.”
Afisa huyo alisema kwamba, wote wanaodhani TRA imezikomoa kampuni hizo kwa kuzipa deni hilo, wanakosea kwa sababu deni hilo limetokana na malimbikizo ya ukwepaji kodi.
Taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya Acacia baada ya kupata madai hayo ya TRA ilionyesha kuwa deni hilo la USD 190 bilioni, BGML wanadaiwa USD 154 bilioni na PML wakidaiwa USD 36 bilioni.
Katika USD 190 bilioni, USD 40 bilioni ni malimbikizo ya kodi na USD 150 bilioni zikiwa ni riba na faini kutokana na kukiuka
Post a Comment