Mbowe Amshangaa Spika na Waziri Ummy Mwalimu Matibabu ya Tundu Lissu
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amemshangaa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
kusema kuwa Serikali iko tayari kumtibu Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu popote duniani.
Mbowe
ametoa mshangao huo jana Ijumaa alipokuwa akitoa taarifa kuhusu matibabu
ya Lissu yanayoendelea jijini Nairobi. Amesema wakati walipoamua
kumpeleka Lissu jijini Nairobi, Waziri Ummy alikuwepo lakini walitaka
Lissu apelekwe Muhimbili kwanza na baadaye kama angepata rufaa
angepelekwa nchini India.
“Sasa
wiki mbili baadaye ndio anatoka Waziri wa Afya anasema Serikali iko
tayari kumtibu popote duniani, eh kweli? Mama Ummy Mwalimu anasahau
kauli yao wakinieleza mimi pale Dodoma, wamuogope Mungu, walikataa
‘categorically’ pengine walifikiri wao ni miujiza mheshimiwa Lissu
kupona na sisi tulisema lazima tumpeleke Nairobi ndiyo mahali tunaona
kweli kunawezekana kukaokoa yale maisha,”amesema Mbowe.
“Ilikuwa
ni hatari na ni maamuzi yalikuwa magumu sana, watu ambao wana mamlaka,
Waziri wa Afya yuko pale, Spika yuko pale nawaambia fanyeni maamuzi
tumuokoe huyu mtu wanasema hatuwezi kumpeleka Nairobi, mimi nikasisitiza
sisi tunampeleka Nairobi wakasema basi utalipa mwenyewe, nikasema sawa
tutalipa wenyewe.”
Pamoja
na hayo Mh. Mbowe amesema kwamba Spika wa bunge kupitia wasaidizi wake
alimtafuta siku chache zilizopita na kumtaarifu kwamba Serikali inaweza
kusaidia matibabu ya Lissu lakini kwa masharti matatu, ikiwa ni wakubali
apelekwe India, aandikie barua ya maombi na tatu apeleke taarifa yote
kuhusu matibabu ya hospital ya mgonjwa na kwa upade wake alikataa.
Ameongeza
"Jana Ummy anasema familia iandike maombi siyo chama maana mimi
nilikataa. Wabunge kutibiwa na serikali ni stahiki. Wabunge wengi
wametibiwa kwa nyakati tofauti labda kama ingekuwa anaumwa mtoto wa
Lissu na anatibiwa kwa kofia ya baba yake ndio baba yake angeomba.
Lakini kuhusu mimi kuandika sitaweza kuandika labda Spika ajiandikie
yeye, au familia ya Lissu iandike lakini mimi nimesema kama kiongozi
wake wa chama sitaweza.
Hata
hivyo Mbowe amesema hiyo ni hali halisi ambayo ameona awaambie
Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwashukuru watu mbalimbali waliochangia
matibabu ya Lissu na kuwaomba kuendelea kuchangia matibabu ya Tundu
Lissu.
Post a Comment