Na
Tiganya Vincent,RS-Tabora
KANISA
Katoliki Jimbo Kuu la Tabora limeitaka jamii pamoja katika kuungana katika
kuwalinda ,kuwaheshimu na kusihi nao watu wenye ulemavu wa ngozi ili nao waweze
kutembea kifua mbele katika nchi hii kama walivyo watu wengine.
Kauli
hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki mkoani
Tabora Mhashamu Paulo Luzoka wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku mbili juu ya
kuwahudumia watoto wenye ulemavu wa ngozi.
Alisema
kuwa ni wajibu wa jamii nzima bila kujali tofauti zake za kiimani kushirikiana
na Serikali katika kuhakikisha kuwa haki ya kuishi watu wenye ulemavu wa ngozi
inalindwa na kuwafanya waishi kwa amani na furaha.
Mhashamu
Luzoka alisisitiza kuwa ni vema jamii ikaweka nguvu katika kuelimisha jamii
kuachana na vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye ulemavu kwa imani za
kishirikina ambavyo vinawafanya watu hao wasiishi kama watoto yatima.
Alisema
kuwa hatua hiyo itasaidia kuwafanya waishi bila hofu na hivyo kuwa huru katika
kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yoyote ya nchi hii.
“Tusingependa
kuona kuwa dawa ya watu hao ikendelea kumwagika kwa sababu ya ulemavu wao…jifikie
wewe ungekuwa katika hali hiyo nawe ukatendewa kama wanavyofanyiwa watu hao
ungejisikiaje ? kama wewe unapenda kutendewa jambo jema basi mtende na wewe
albino jambo jema” alisema Askofu huyo wa Jimbo Kuu la Tabora.
Alisisitiza
kuwa kama jamii itaungana na kuishi kwa amani basi hakutakuwepo na mauaji ya
watu wenye ulemavu na wazee kwa sababu ya umri wao kuwa mkubwa na macho
kubadilika.
Awali
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alilishukuru Kanisa kwa mpango wa
kukabiliana na unyanyapa kwa watoto wenye ulemavu katika jamii wakiwemo albino.
Alisema
kuwa Serikali ya Mkoa wa Tabora itasimama imara kukabiliana na tatizo hilo
ikiwemo kuwakata watu wote wenye imani za kishirikina ambayo wamekuwa wakimwaga
damu za watu wenye ulemavu wa ngozi kwa mawazo ya kijinga kuwa watapata
utajiri.
Post a Comment