Mechi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC dhidi ya Singida United itakayochezwa Novemba 4 mwaka huu katika mzunguko wa tisa wa michuano ya ligi kuu ndiyo itakayozindua rasmi uwanja wa Namfua mkoani Singida.
Uwanja huo ambao umefungwa kwa muda ili kupisha matengenezo yaendelee, na utakapofunguliwa utatumika kama dimba la nyumbani kwa timu ya Singida United ambayo kwa sasa inatumia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma katika michuano inayoendelea ya ligi licha ya makazi yake kuwa mkoani Singida.
Akizungumza Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba ambaye ndiye mdau mkubwa katika matengenezo hayo, amewahakikishia wapenzi wa kandanda mkoani humo kuwa uwanja huo utakuwa tayari kabla ya Novemba 4, 2017 na kuwataka wakazi wa Singida kujiandaa kuishangilia timu yao.
Kwa mujibu wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Singida United imeweza kushika nafasi ya tatu kwa alama tisa ikiwa mbele kwa alama moja dhidi ya Yanga SC ambayo imeshika nafasi ya sita kwa pointi nane.
Post a Comment