Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

RC NDIKILO -AKEMEA MFUMO WA KANGOMBA NA CHIBUDA AMBAO HUWAKANDAMIZA WAKULIMA WA ZAO LA KOROSHO

korosho
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,amekemea biashara ya korosho kufanywa katika mfumo wa kangomba na Chibuda,ambao huwakandamiza wakulima wa zao hilo.
Amesema korosho zote zitakazokutwa kwenye magari yatakayokamatwa yakiwa kwenye mifumo isiyo rasmi badala ya stakabadhi ghalani ambao unatambulika ,korosho zitataifishwa  na mtuhumiwa atakamatwa na jeshi la polisi.
Akizungumzia juu ya zao la biashara la kimkakati mkoani hapo,mhandisi Ndikilo,alieleza kwamba mbali ya kutaifisha korosho pia mtuhumiwa atatakiwa kutoa faini .
Alisema wakulima wa korosho wasikubali kurubuniwa na madalali ama wanunuzi wachache ambao hutumia jasho lao kujinufaisha .
Mkuu huyo wa mkoa ,alielezea kuwa,anaedhani atatengeneza fedha kwa kutumia mifumo hiyo amechelewa kwani msimu huu hatotaka kuona mkulima wa korosho anakandamizwa kimaslahi .
Mhandisi Ndikilo,alitoa wito kwa wakulima kuunga mkono uhamasishaji wa mfumo wa stakabadhi ghalani  ili kuongeza tija na kasi ya kukuza zao hilo la kimkakati mkoani humo.
“Mfumo huu unarahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi za korosho kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo ya tasnia ya korosho huku ukipunguza wimbi la madadali wanaonunua korosho na kutorosha kwa njia ya magendo”alisema mhandisi Ndikilo.
Alisema mfumo wa stakabadhi ghalani hukusanya mazao kwenye ghala maalum lililosajiliwa na serikali kwa lengo la kuyauza kwa bei ya ushindani,na kumkomboa mkulima wa korosho.
Mhandisi Ndikilo,alisema mwaka 2015-2016 wakulima waliweza kuuza korosho zao grade ya kwanza sh.2,900 kwa kilo ,hivyo wanatarajia msimu huu korosho nyingi zitauzwa kwa bei nzuri na kutopata changamoto zinazokuwa zikiwakabili wakati wa soko.
Aidha aliwataka wataalamu wa zao la korosho kusimamia wakulima hao kupanda miche mipya ya mikorosho.
Baadhi ya wakulima katika wilaya ya Kibiti na Rufuji ,waliomba serikali ya mkoa huo kuendelea kuwapigania katika changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara kwa mara hasa wakati wa kuuza korosho zao.
Walisema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya makampuni yanayonunua korosho zao ,kuchelewesha malipo ,ama kuweka dosari ambazo huwakatisha tamaa .
Mikoa ya Ruvuma na Pwani ilianza kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika msimu wa mwaka 2009/2010 kwa lengo la kumuinua mkulima wa zao hilo.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget