Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dk. Chrales Msonde.
NA CHRISTINA
MWAGALA, Dar
WANAFUNZI 917,072
wa darasa la saba kutoka shule za Msingi 16,583 wanatarajiwa kufanya mtihani wa
kumaliza elimu ya msingi kesho Jumatano na Alhamisi.
Kati ya
wanafunzi hao, inadaiwwa kuwa wavulana
ni 432,744 sawa na asilimia 47.19 , huku wasichana wakiwa 484,328 sawa na asilimia
52.81.
Akizungumza na
waandishi wa habari jiji Dar es Salaam mapema leo asubuhi, Katibu Mtendaji wa
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dk. Charles Msonde amesema kuwa
watahiniwa hao watafanya mtihani wa masomo ya Kiswahili, Englishi Language,
Sayansi, Hisabati na Maarifa ya jamii.
Dk. Msonde
amesema kati ya watahiniwa 917, 072 waliosajiliwa kufanya mtihani huo, watahiniwa
882,249 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 34,823 watafanya
mtihani kwa lugha ya Kingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia.
Amesema kuwa
watahiniwa wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani huo ni 94 wakiwemo wavulana
58 na wasichana 36, huku watahiniwa wenye uoni hafifu ambao huhitaji maandishi
makubwa wapo 1,138 ambao pia wavulana ni 586 huku wasichana wakiwa 552.
Dk.Msonde
amesisitiza kwamba maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa
ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mitihani , fomu maalumu za OMR,
zakujibia mtihani na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo katika
halmashauri zote hapa nchini.
“ Mtihani wa
kumaliza elimu ya msingi ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla, kwa kuwa
hupima uwezo na uelewa wa wanafunzi katika yale yote waliojifunza kwa kipindi
cha miaka saba” amesema Dk. Msonde.
Aidha Dk. Msonde
ametoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha kuwa
taratibu zote za uendeshaji wa mitihani wa Taifa zinazingatiwa ipasavyo ikiwa
ni pamoja na kuhakikisha kwamba mazingira ya vituo hivyo yapo salama.
“ Baraza pia
linatoa wito kwa wasimamizi wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa
hali ya juu ,pia wajiepushe na vitendo vya udanganyifu, atakaye bainika
hatutasita kumchukulia hatua” amesisitiza Dk. Msonde.
Hata hivyo
Dk. Msonde aliwakumbusha wamiliki wa shule kutambua kwamba shule zao ni vituo
maalumu vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya
wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyikaji wa mitihani.
|
Post a Comment