Waziri Mwijage
Mh. Mwijage ameyasema hayo jana ambapo amedai kuwa anaoushahidi kuwa kampuni hizo za udalali zilivyochafua jina la nchi hivyo ni lazima awafikishe katika mikono yua sheria.
“Vitendo hivi vinavyofanywa na makampuni haya havivumiliki kwani mchezo huu ni mauti kwetu na nitahakikisha wanachukuliwa hatua kwani ninao ushahidi unaotosheleza,”alisema Mwijage.
Mh. Mwijage amefafanua kwa kusema kwamba watu wametapeliwa kwa kuambiwa pindi wanapoagiza mazao kuwa watoe pesa ya kianzio ambayo ni kuanzia dola za Marekani 123,000, sawa na Sh275 milioni na dola 200,000 sawa na Sh448milioni za kitanzania.
“Nimepokea wito kutoka India kwa ajili ya kwenda kusafisha jina la nchi kutokana na taswira ilisababishwa uwepo wa matapeli hao,”alisema Mwijage.
Post a Comment