Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

BANDARI BUBU NDIO CHANZO CHA KUPITISHA MADAWA YA KULEVYA VISIWANI PEMBA


FB_IMG_1463725614003
Na  Masanja Mabula –Pemba …
SUALA la bandari bubu ni moja ya agenda ilizotawala mkutano wa nne wa wakuu wa Mikoa iliyo katika mwambao wa bahari ya Hindi  ya Tanzania Bara na Zanzibar uliofanyika  katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mkoa wa Kaskazini Pemba .
Wakuu hao wa Mikoa wamesema bandari hizo ndizo ambazo zinatumika kupitisha madawa ya kulevya , magendo ya karafuu na mafuta , uingiaji wa wahamiaji haramu ndani ya nchi pamoja na kusafirisha abiria na mizigo jambo ambalo linapoteza mapato ya Serikali .
Akifungua mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ameitaja mikoa ya Pemba pamoja na Tanga ndiyo inayoathirika zaidi na bandari hizo kwani  asilimia kubwa hutumika katika kupitisha dawa za kulevya  na wahamiaji haramu .
Amesema kuwa matukio mengi ya kupotea kwa raia wa Somalia wanaokotwa katika Wilaya ya Micheweni  Mkoani hapa  na kushangaa kuona wasomali hao  wakipotea hupotelea katika Mkoa wa Kaskazini Pemba jambo ambalo linahitaji kuchukuliwa hatua za haraka  ili lidhibitiwe.
“Maeneo ya mikoa yetu kwa kweli yako hatarini kutokana na kuwa wazi jambo ambalo linasababisha madawa ha kulevya kupitishwa , magendo kusafirishwa pamoja na kuingia wahamiaji haramu , wakati umefika wa kuimarisha ulinzi katika maeneo ya bandari bubu ”alisema.
Ameeleza kwamba katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kuna bandari Bubu 162 kati ya hizo 88 ziko Wilaya ya Wete na 74 ziko Wilaya ya Micheweni  , ambazo asilimia kubwa zinatumika kuptishia vitu ambavyo vinahatarisha usalama wa maisha ya wananchi na mali zao .
Akitoa taarifa ya Bandari bubu , Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama ZMA Msilimiwa Idd Msilimiwa amesema kisiwa cha Pemba pekee kina jumla ya bandari bubu 479 wakati m ikoa ya Tanzania Bara ikiwemo Tanga , Pwani , Dar es Salaam , Lindi na Mtwara kuna bandari bubu 99.
Amesema kwa mikoa ya Tanzania Bara Mkoa wa Pwani unaongoza kwa kuwa na bandari Bubu 35 ukifuatiwa na Mkoa wa Tanga wenye bandari bubu 32 , Dar es Salaam na Mtwara kila mmoja auna bandari bubu 8 na mkoa wa Lindi una bandari 16.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Engineer Evasrto Ndikiro amezitaka SUMATRA  pamoja na TPA kuitupia jicho la pekee bandari ya Bagamoyo kwani ni  bandari  ambayo inaweza kuingizia serikali fedha za kutosha .
Amesema Bandari ya Bagamoyo inauwezo wa kuingiza shilingi bilioni moja kwa mwezi , fedha ambazo kama kungekuwa na udhibiti mzuri kutoka mamlaka husika zingeweza kutumika katika masuala mbali mbali ya kijamii .
“Bandari ya Bagamoyo inauwezo wa kuingiza shilingi bilioni moja kwa mwezi , lakini fedha hizi zinashindwa kuingia kwenye mifuko ya Serikali kutokana na kukosekana kwa udhibiti mzuri wa mapato katika bandari hiyo ”alieleza.
Hivyo amewashauri viongozi wa Mkutano huo kuangalia uwezekano wa kununua boti ya mwendo kasi ambayo itakuwa inafanya doria za mara kwa mara katika mwambao wa bahari ya hindi ili kudhibiti vitendo vya uhalifu .
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget