Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

SIMBA FC YAFANIWA KUTINGA FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO, BAADA YA KUIFUNGA AZAM FC


 Image result for picha za timu ya simba sc




SIMBA SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho, linalojulikana kama Azam Sports federation Cup baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya 48, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim ambaye hata hivyo hakumaliza mchezo baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu baadaye.

Kwa ushindi huo, Simba itasubiri kukutana na mshindi kati ya wenyeji Mbao FC na Yanga SC zinazomenyaa kesho Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mathew Akrama wa Mwanza, Azam FC ilipata pigo dakika ya 15 baada ya kiungo wake mchezeshaji, Salum Abunakar ‘Sure Boy’ kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib.

Lakini kwa namna Hajib alivyojirusha huku akipiga yowe la kuugulia maumivu Akrama aliingia kwenye mtego wa kumtoa kwa kadi nyekundu Sure Boy.

Tukio hilo lilileta kizaazaa kidogo uwanjani baada ya wachezaji wa Azam kumfuata refa na kuanza kumlalamikia kwa maamuzi yake. Walinzi wa Uwanja wa Taifa walimfuata Sure Boy na kujaribu kumtoa kwa nguvu, jambo ambalo liliwafanya wavutane na Meneja wa Azam, Philipo Alando.
 
Mchezo uliendelea baada ya tukio hilo, huku timu zikiendelea kushambuliana kwa zamu na kabla ya Akrama kupuliza kipyenga cha kumaliza ngwe ya kwanza kukiwa hakuna bao.

 
Kipindi cha pili, Simba walikianza vizuri na kufanikiwa kupata bao baada ya dakika tatu tu, kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim akimtungua vizuri kipa Aishi Salum Manula kwa shuti la mguu wa kulia kufuatia ya krosi ya mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo.


 
Simba wakaanza kucheza kwa tahadhari kwa kujihami zaidi baada ya bao hilo, huku Azam FC wakionekana kusaka bao la kusawazisha kwa nguvu zao zote.

 
Mo Ibrahim akaonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 77 baada ya kumchezea rafu beki wa Azam FC, Shomary Kapombe.

 
Beki Mkongo, Janvier Besala Bokungu akaizuia Azam FC kusawazisha baada ya kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na Nahodha wa timu hiyo, John Raphael Bocco uliokuwa unaelekea nyavuni dakika ya 84.

 
Kikosi cha Simba kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, James Kotei/Said Ndemla dk88, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo/Mwinyi Kazimoto dk86, Ibrahim Hajib na Mohammed Ibrahim.

 
Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Daniel Amoah, Himid Mao, Stephan Kingue/Joseph Mahundi dk58, Shaaban Iddi/Frank Domayo dk46, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Ramadhani Singano ‘Messi’/Mudathir Yahya dk82
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget