Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WANANCHI KATA YA KILANGALA WAMETAKIWA KUJIKITA KWENYE KUBORESHA MAENDELEO NA SIO PROPAGANDA



MBUNGE wa Jimbo la Mchinga mkoa wa Lindi, Hamidu Bobali CUF, amewataka wananchi wa Kitongoji cha Lichinji kata ya Kilangala kuachana na propaganda na kujikita katika kuboresha huduma za jamii na maendeleo.

Bobali aliyasema hayo jana katika mkutano na wanakitongoji huo ambao ulibeba ajenda ya ujenzi wa shule ya awali ya Kiwalala ambayo aliahidi kujenga.

Alisema ni jambo la kusikitisha na aibu kuona bado wapo viongozi wa kisiasa ambao wanaendekeza propaganda badala ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo ya Kitongoji.

Alisema mitazamo ya u CCM na u CUF inapaswa kuondolewa ili kuweza kutekeleza malengo ya wananchi ambao wamewakabidhi majukumu.

"Kusema kweli inanikera kusikia kuwa ujenzi wa shule ya awali ya Kiwalala unakwamishwa na watu ambao wanaendekeza propaganda za vyama ni aibu na tunapaswa kuwatenga," alisema.

Alisema elimu ndio ukombozi wa watoto hivyo ni vema kuungana na kumuona mtu ambaye anakwamisha elimu kama mchawi hivyo kumuogopa na kutenga.

Bobali alisema matarajio yake ni kuona shule hiyo ya awali inaanza kutumika mapema mwakani huku akiahidi kuwshirikisha wadau mbalimbali kusaidia ujenzi.

Kwa upande mwingine mbunge huyo ametoa rai kwa vijana kujikita katika kilimo cha korosho huku akibainisha kuwa kinalipa zaidi ya mazao mengine.

Bobali alisema katika msimu uliopita kilo ya korosho imeuzwa zaidi ya sh. 3500 bei ambayo haijawahi kutokea tangu zao hilo lianzishwe.

Alisema jitihada za bei kufikia hapo zimechangiwa na ushirikiano uliopo kwa wabunge wao bila kuangalia itikadi za vyama vyao na kuahidi kuwa mkakati wao ni kuona bei inaongezeka zaidi.

Alisema wao wamekubaliana kwa pamoja kuwa wakijadili maslahi ya wana Lindi vyama havina nafasi jambo ambalo linasaidia kufikia muafaka hivyo vijana wanapaswa kulima kwa nguvu zote zao la korosho ili kujiajiri.

Mbunge huyo alisema katika mauzo ya msimu uliopita korosho imeingizia mkoa wa Lindi umeingiza zaidi ya sh.bilioni 166 na halimashauri ikifanikiwa kupata zaidi ya sh.milioni 850 kama ushuru.

Diwani wa Kata ya Kilangala Kassim Namwete alisema ofisi yake imejipanga kushirikiana na mbunge kwa maslahi ya wananchi wa kata hiyo.

Alisema changamoto kubwa ilikuwa eneo la kujenga ila Mwenyekiti wa Kitongoji Mohamed Mpwatile ametoa eneo na ujenzi unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Mwenyekiti Mpwatile alisema ametoa eneo hilo kwa kuwa anaamini faida ya elimu pamoja na kuunga mkono jitihada za mbunge wao.

Mpwetele alisema msaada wa mbunge wa mifuko 50 ya saruji imefanikisha kufatuliwa matofali 1500 ambayo yatatumika kwa ujenzi wa shule hiyo.

Diwani wa Viti maalum CUF, Somoe Hassan alitoa wito kwa wananchi wa kitongoji hicho kupigania maendeleo hasa kwa kumuunga mkono mbunge wao ambaye ameonesha jitihada kubwa kuwapigania.

Mkazi wa kitongoji hicho Ibrahim Tondoro alitoa wito kwa wananchi wenzake kujitokeza wakati wa ujenzi ili shule hiyo iweze kukamilika.A
 MBUNGE wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi Hamidu Bobali akizungumza na wananchi 106 wa Kijiji cha Kilangala B kata ya Kilangala ambao wanadai fidia ya kuunguliwa na mimea yao katika mashamba yao wakati wa mradi wa kupitisha bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam. Kulia ni DIWANI viti maalum CUF Somoe Hassan,Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akifutiwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mohamed Ng'aka (Picha na MPIGA PICHA wetu).

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget