Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

MWAMBUSI-TUNATAKA MAKOMBE YOTE LIGI KUU NA FA


Kocha-Mwambusi-640x426
Na.Alex Mathias
Baada ya kikosi cha Yanga kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu George Lwandamina raia wa Zambia pamoja na Msaidizi wake Juma Mwambusi wameweke wazi  kuwa mipango yao ni kuhakikisha kikosi hicho kinatwaa mataji mawili msimu huu; ligi kuu na Kombe la FA.
Yanga walitinga hatua hiyo baada ya kuiondosha Prisons ya Mbeya kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar juzi Jumamosi huku mabao yakifungwa na washambuliaji tegemeo kwa sasa Amis Tambwe,Obrey Chirwa na Simon Msuva.
Huku wakiwa na matumaini ya kunyakuwa ubingwa wa Ligi kwa mara ya tatu mfululizo wakiwa wanamechi tano huku watani zao wamebakiwa na mechi tatu na wakiwa na pointi 59 na Yanga 56 endapo Simba watashinda michezo yote miwili watafikisha pointi 68 huku Yanga wakihitaji kushinda mechi tatu na sare moja hata wakifungwa mmoja watakuwa na pointi 69 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Kocha msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi, amesema kuwa, wanataka makombe hayo kwa ajili ya kupooza machungu waliyonayo baada ya kutolewa kwenye michuano ya kimataifa ambako walielekeza nguvu zao msimu huu.
“Nguvu kubwa ilikuwa ni kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, lakini kila kitu kiligeuka ndoto baada ya kutolewa, hivyo akili zetu ni kuhakikisha tunachukua makombe yaliyobakia hapa nyumbani.
Msimu huu Yanga haukuwa mzuri kutokana na matatizo yaliyompta Mwenyekiti wao Yusuf Manji suala ambalo limesababisha wachezaji kukosa morali ya kujituma huku wakicheza bila kulipwa madai yao na kusababisha kufanya vibaya katika ngazi zote za CAF kwani waliweza kutolewa na Zanaco FC kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kombe la Shirikisho ambapo napo walitolewa na MC Alger na kutupwa nje ya mashindano.
“Tuna nafasi nzuri kwenye ligi, japo Simba wapo juu yetu kwa sasa, hilo halituogopeshi sana kwani tukishinda mechi zetu za viporo, mambo yatakuwa sawa, pia tunataka kufanya vizuri katika FA kwa ajili ya kujihakikishia nafasi ya kutinga michuano ya kimataifa msimu ujao,” alisema kocha huyo.
Yanga watakuwa wageni wa Mbao FC siku ya Jumapili April 30 kucheza nusu Fainali itakayopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kabla ya kuwavaa wapasua mbao hao tayari watakuwa wameshajua wanaweze kukutana na nani endapo watatinga Fainali hiyo kwani April 29,kwemye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam vinara wa Ligi Simba watacheza na Azam FC
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget