Image caption
Saul Niguez's header was only the second home goal
Leicester have conceded in the Champions League this season
Safari ya Leicester
City katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu imefikia kikomo baada
ya klabu hiyo ya Uingereza kutoka sare na Atletico Madrid uwanjani King
Power.
Walitawala mechi hiyo katika uwanja huo wa nyumbani na wakaunda nafasi nyingi za kufunga.
Hata hivyo, walijipata wakiwa na mlima wa kukwea baada ya Saul Niguez kufunga bao kwa kichwa dakika ya 26.
Hilo lilikuwa na maana kwamba walihitaji angalau mabao matatu kipindi cha pili ili kufanikiwa kusonga.
Jamie Vardy alikomboa bao moja dakika ya 61 lakini Atletico walifanikiwa kujilinda hadi dakika ya mwisho na kuhakikisha wanajiunga na Real Madrid kwenye nusufainali.
Real waliwalaza Bayern Munich ya Ujerumani 4-2 na kupata ushindi wa jumla wa 6-1.
Image caption
Atletico Madrid wamefungwa mabao matatu pekee mechi zao 10 walizocheza karibuni mashindano yote
Post a Comment