
Na. Catherine Sungura, WAMJW
Ujumbe wa wawekezaji toka nchini
Misri wamewasili nchini hapa na kufanya mazungumzo na serikali ya
Tanzania kwa nia ya kujenga viwanda vya dawa za binadamu zikiwemo za
majimaji pamoja na zile za antibiotic.
Ujumbe huo ulikutana jana na
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
pamoja na wawakilishi toka wizara Viwanda,Biashara na Uwekezaji na Kituo
cha Uwekezaji cha Taifa (TIC) kwenye ofisi ndogo ya wizara ya
afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto iliyopo jijini Dar es
Salaam
Ujumbe huo ulisema kuwa kiwanda
walichokusudia kujenga nchini hapa kitazalisha dawa za majimaji yaani
“IV Fluids” pamoja na “antiobiotics” za aina mbalimbali ikiwemo
“Paracetamol IV” na dawa za kutibu Malaria
Aidha, walisema lengo lao ni
kujenga kiwanda kikubwa ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha dawa
ambazo zitawahudumia watanzania pamoja na nchi za Afrika Mashariki na ya
kati.
Katika mazungumzo hayo,wawekezaji
hao pia wanatarajia kusaidia Tanzania katika uzalishaji wa chanjo ya
ugonjwa wa homa ya Ini (Hepatics B na C ).
Kwa upande wake Waziri Ummy
amewaahidi wawekezaji hao kuwasaidia katika mipango ya ujenzi huo na
kutoa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha viwanda hivyo vinajenga
nchini kwa muda uliopangwa.
“naelekeza kwa taasisi zote
zitakazoguswa na uanzishwaji wa viwanda hivi watoe ushirikiano wa hali
ya juu ili lengo hili lifikiwe,soko la dawa hapa nchini lipo naomba
niwahakikishie hili”alisema waziri Ummy.
Waziri Ummy aliwaomba wawekezaji
hao kuharakisha ujenzi wa viwanda huo na kujengwa ndani ya miezi kumi na
nane kama walivyoahidi ili watanzania waanze kunufaika mapema.
Post a Comment