
Na Masanja Mabula –Pemba
MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ameuagiza Uongozi wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Tawi la Kangagani Wilaya ya Wete kushirikiana katika kazi za ukarabati wa Ofisi za Tawi hilo lililozeluwa na upepo ili ukamilike kwa wakati .
Amesema kila mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Tawi hilo anapaswa kushiriki kikamilivu katikia kufanikisha ukarabati wa Tawi lao kwa kuchangia misaada mbali mbali ya hali na mali ikiwa ni pamoja na nguvu kazi .
Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kutembelea Tawi hilo lenye Historia ndevu ya Chama hicho Kisiwani Pemba , Mjumbe huyo wa Kamati ya Siasa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba amewaomba wanaCCM kuwa wazalendo na chama chao kwa kushiriki kazi kwa kujitolea .
Amesema pamoja na wahisani wengine kutoa michango yao lakini ni vyema wanachama wa chama cha Mapinduzi wa Tawi kuguswa na tukio na kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha linaezekwa .
“Pamoja na wahisani kutoa michango yao kukarabati tawi hili , lakini kila mwanachama anapaswa kuguswa , hivyo ni lazima kujitolea kuchangia ukarabati wake kwani linahostoria kubwa katika ukombozi wa Visiwa vya Zanzibar ”alisisitiza.
Aidha Mjumbe huyo wa kamati ya Siasa amesema Serikali ya Mkoa wa Upande wake itashirikiana na wanachama wa Tawi hili katika ukarabati wake ili ukamilike kwa wakati na kutoa fursa kwa wanachama kuendesha shughuli zao za chama wakiwa sehemu tulivu .
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Wete ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Rashid Hadid Rashid amewataka wana CCM wa tawi hilo kutambua kwamba ukarabati wa tawi hilo utafanyika na kukamilika kwa wakati muafaka .
Amesema yeye binfasi pamoja na Serikali ya Wilaya watasimamia ili kuona wanachama wa CCM kwa kila mmoja anakuwa msitari wa mbele katika kutoa michango yake .
Katibu wa Tawi hilo Hamad Said amesema kuwa kuezeliwa kwa tawi hilo kumerudishwa nyuma harakati za maandalizi ya uchaguzi wa chama kutokana na kukosekana sehemu ya kuwatanisha wanachama wote.
Ameeleza kwamba pamoja na changamoto hiyo , lakini uongozi wa chama Tawi umefanya juhudi za makusudi kukamilika ukabarati huo kabla ya kuanza mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama .
“Tunaendelea kupokea michango na misaada kutoka sehemu mbali mbali , na tunakusudia kukamilika ukabarati huu kabla ya kuanza mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama licha ya kwamba kwa wanachama wamekosa sehemu ya kukaa na kupanga mipango yao ”alieleza.
Tawi la CCM Kangagani limezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua na kusababisha baadhi ya kuta za jengo hilo kupasuka .
Post a Comment