
Baraza la Wafanyakazi
linaundwa kwa mujibu wa matakwa ya kisheria ya uwepo wa Baraza la
Wafanyakazi mahali pa kazi ambalo linaendesha shughuli zake kwa
kuzingatia Mkataba wa Baraza la wafanyakazi.
Kwa kutambua hilo, Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Jinsia,Jinsia
Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis A. Kingwangala amefungua Mkutano wa
Baraza la Wafanyakazi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii uliofanyika
Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kukuu cha Dodoma kwa ili kujadili na kutoa
maoni kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara kwa mwaka 2016/17 na
mpango na bajeti ya wizara 2017/18.
Akifungua mkutano huo, Mgeni
rasimi Mhe. Kigwangalla alipongeza viongozi wa TUGHE kuanzia ngazi ya
Tawi hadi Taifa kwa kudumisha mahusiano rafiki mahala pa kazi, na kuweza
kutoa ushauri ambao umesaidia kuaminiana na kuimarisha mahusiano baina
ya menejimenti na wafanyakazi wa Wizara.
Mhe. Naibu Waziri ametoa rai
kuwa, ili kufikia dira, dhima na malengo ya Wizara tunahitaji kuwa na
mpango na bajeti inayozingatia utekelezaji wa vipaumbele vilivyowekwa.
Kwa kutambua hilo Bajeti ya Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii imeaandaliwa
kwa muktadha huo, na pia inaakisi sera, mipango, mikakati ya Taifa,
Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala na mikataba ya Kikanda na Kimataifa.
Katika kufanikisha malengo
hayo ya Mhe. Naibu Waziri amesisitiza kila mtumishi kufanya kazi kwa
bidii na maarifa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi
wa umma. Na pia Wizara amesisitizwa kuendelea kutoa motisha kwa
watumishi wanaowajibika, wabunifu na wenye maadili mema ili kuwa
kichocheo cha ubunifu, tija na ufanisi sehemu ya kazi.
Naibu Waziri ameipongeza
Wizara kwa kufanikiwa kuandaa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi na
kuwataka kutumia weledi na umahiri wa watumishi kukabiliana na
changamoto zilizopo na kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara
ambayo ni pamoja na kuelimisha jamii kuondokana na mila na desturi zenye
madhara kama ukeketaji ambao sasa tuna asilimia 10 na ndoa za utotoni
asilimia 37; kuamsha ari ya jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo
na ustawi wao; kufanya ufuatiliaji wa mashirika Yasiyo ya Kiserikali
ili kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na taratibu. Aidha,
ameelekeza Wizara kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa
Kudhibiti Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ambao
tumejipangia kupunguza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2025.
Mhe. Kigwangala amebainisha
mambo manane ambayo Wizara inatakiwa kuyazingatia. Mambo hayo ni
kutimiza haki na wajibu kwa kila mtumishi kutoa mchango wa mawazo na
ushauri kwenye utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17 na Mpango na
Bajeti ya mwaka 2017/18. Pili, kushiriki kujadili changamoto za
kiutekelezaji na kuzibadili kuwa fursa kwa kutoa ushauri na mapendekezo
ya namna ya kuboresha utendaji. Tatu, kutekeleza majukumu kwa mujibu wa
sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma. Nne, kuitikia
utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake
na Watoto kusimamiwa ipasavyo na shirikishwa wa wadau wote.
Maeneo mengine ni kuhakikisha
kuwa Wataalam wa wizara wanashirikiana na OR TAMISEMI ili kuhuisha ari
ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo yao. Sita, kuimarisha
mahusiano na OR TAMISEMI ili kuhakisha wataalam waliopo kwenye ngazi za
Mikoa na Halmashauri wanatumika na kutekeleza majukumu ipasavyo. Saba,
Vyuo vya maendeleo ya jamii kutoa elimu inayoandaa wataalam wenye weledi
na mahiri katika kutekeleza kazi za maendeleo ya jamii. Mwisho,
Watumishi kuwa na hadhari na tabia hatarishi zinazopelekea maambukizi ya
ukimwi na kwa upande mwingine mwajiri aendelee kutoa huduma kwa
wathirika kwa mujibu wa bajeti.
Mapema akimkaribisha Mgeni
Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee
na Watoto, Bibi Sihaba Nkinga alimfahamisha Mgeni Rasimi kuwa, wajumbe
wa Baraza la Wafanyakazi watajadili Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa Fedha
2017/18. Kwa mujibu wa Sheria inayounda mabaraza ya wafanyakazi mahali
pa kazi kwani ni lazima Bajeti ya Wizara ipitishwe na Baraza la
Wafanyakazi. Agenda ya pili, ilikuwa kupitia na kufanyia marekebisho
muundo wa Baraza ili kujumuisha Idara ya Ustawi wa Jamii,
iliyounganishwa kutoka Idara Kuu ya Afya, baada ya mabadiliko ya muundo
wa Wizara. Aidha, baada ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kuhamia
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Wizara imeona kuna umuhimu wa
kuwa na wawakilishi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
kwa uwakilishi wa menejimenti na uwakilishi wa watumishi.
Katibu Mkuu Sihaba, alifafanua
tunu za Wizara kwamba, ari waliyonayo watumishi katika kutimiza
majukumu yao kwa weledi, uadilifu, juhudi na maarifa katika kuchangia
maendeleo na ustawi endelevu wa Taifa. “Katika hili tumeendelea
kuhamasisha jamii na kutoa elimu kuhusu maendeleo na ustawi wa jamii,
usawa wa kijinsia, uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali na
maendeleo ya mtoto kwa jamii, maafisa wa serikali na wadau wengine wa
maendeleo”. alisema.
Kitengo cha Mawsiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Idara Kuu ya Mendeleo ya Jamii
Post a Comment