
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania
Health Summit Bi. Rebecca John (katikati) akisisitiza jambo kwa
wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio
za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali
kupunguza magonjwa yasiyoambukizika mapema hii leo jijini Dar es Salaam,
kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni
Zavara na kulia ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam
Bw. Lucas Nkungu.

Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha
Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara akizungumza na wandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya
yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika
mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya
Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania
Health Summit Dkt. Omary Chillo (kulia) akifafanua jambo kwa wandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za heart
marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza
magonjwa yasiyoambukizika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati
ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu
na kushoto ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi.
Rebecca John.
……………..
Na Nuru Juma-Maelezo
Taasisi ya Tanzania Health Summit
yaandaa mbio za nusu Marathon na Upimaji wa afya kwa lengo la kusaidia
juhudi za serikali katika kupunguza magonjwa yasioambukiza, mbio hizo
zinazotarajia kufanyika Aprili 26 katika barabara ya Kaole iliyopo
Masaki jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu
wa Taasisi hiyo Rebecca John wakati alipokutana na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki.
“Kamati ya maandalizi ya ya mbio
za Heart Marathon inapenda kuwa taarifu wadau wote wa sekta ya afya hapa
nchini na jamii kwa ujumla juu ya mbio za Heart Marathon na upimaji wa
afya ili kuungana na serikali katika juhudi za kupunguza magonjwa
yasiyoambukiza” alisema Rebecca.
Aliongeza kuwa kwa mwaka huu mbio
hizi zitashirikisha washiriki zaidi ya elfu mbili kutoka rika mbalimbali
wakiwemo vijana, watoto, wazee, makundi ya watu wenye ulemavu na watu
wenye magonjwa yasiyoambukiza.
Pia washiriki watapata nafasi ya
kupima afya magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo la damu ,wingi wa
sukari katika damu, kiasi cha mafuta mwilini, uchunguzi wa uvimbe katika
matiti na kupata ushauri wa wataalam kuhusiana na vyakula bora,
magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
Aidha Bi. Rebecca aliongeza kuwa
washiriki watakimbia umbali tofauti, kwani kuna mbio ndefu za kilometa
21.1 kwa ajili ya wakimbiaji wazoefu, kilometa 10 kwa wakimbiaji wa
kati, kilometa 5 kwa wakimbiaji wa kawaida, kifamilia na kampuni na mbio
za watoto chini ya miaka 12 ni meta 700 na zawadi itatolewa kwa mshindi
wa kilometa 21.1 pekee kwa kiasi cha shilingi laki tano.
Kwa upande wake Rais wa Tanzania
Health Summit Dr.Omary Chillo alisema kuwa washiriki watatakiwa kutoa
kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kununua flana pamoja na kifaaa
maalum cha kuhesabia muda wakati wa kukimbia ila maji ya kutosha
yatatolewa bure kwa ajili ya wakimbiaji.
Aliongeza kuwa wameimarisha ulinzi
kwa kushirikiana na jeshi la polisi na ili kulinda usalama kwa
washiriki na wananchi watakaokuwepo katika mashindano hayo.
“wananchi wasiwe na wasiwasi wa
usalama kwani tutashirikiana na jeshi la polisi ili kuimarisha usalama
na tumeweza kupata baraka nyingi kutoka kwao kwa kuweza kushirikiana
nao” aliongeza Chillo.
Pia Katibu msaidizi wa Chama cha
Riadha nchini Bi Ombeni Zavala alisema anashukuru wananchi wanavyoweza
kujitokeza katika mashindano hayo na pia anawaomba wananchi hasa vijana
waendelee kujitokeza kwa wingi kwani wanaweza kupata nafasi ya kuunda
timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17.
Naye Sajenti Isaya Mlokozi kutoka
kanda ya usalama barabarani alisema jeshi la polisi kikosi cha usalama
barabarani litahusika vizuri katika sehem inayowahusu kuhakikisha watu
wanafanya zoezi hilo kwa hali ya usalama na litajumuika na wananchi
popote pale watakapokuwa wanakwenda.
Mashindano haya mwaka jana
yalifanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam lakini kutokana na
kuongezeka kwa watu mwaka huu yatafanyikia barabara ya kaole yenye kauli
mbiu ‘piga hatua moja mbele ya magonjwa sugu’
Post a Comment