
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya
Musomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na
usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya
Musomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na
usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi
wa Uhusinano na Mipango wa TPDC, Nathan Mnyawami.

Baadhi ya waaandishi wa habari
wakifuatilia mkutano baina yao na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC
Mhandisi Kapuulya Musomba (hayupo pichani) uliofanyika Ofisini kwake leo
Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija
…………..
Na: Frank Shija – MAELEZO.
TPDC kwa kushirikiana na Sekta
binafsi wanatarjia kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji wa gesi
asilian katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na baadhi ya
mikoa mingine itakayoidhinishwa.
Hayo yamebainishwa na Kiamu
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba wakati akizungumza
na waandishi wa habari Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Musomba amesema kuwa
miradi hiyo imeanza kwa kupitia upya taarifa ya awali ya upembuzi
yakinifu wa mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba la kusambazia gesi
asilia katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo mnamo mwezi machi 22, 2017
TPDC ilikaribisha jumla ya makampuni 9 ambayo yalikidhi vigezo vya
kimanunuzi kwa ajili ya kazi hiyo.
“Napenda kuutaarifu umma kuwa TPDC
inatarajia kutekeleza miradi mbaimbali ya usambazaji wa gesi asilia
katika mikoa ya Dar es Salaam, Bagamoyo na Mkuranga Mkoani Pwani, Lindi
na Mtwara pamoja na baadhi ya mikoa mingine,” alisema Mhandisi Muyomba.
Aliongeza kuwa lengo la kupitia
upya taarifa za awali ni kuboresha zaidi taarifa za kifedha, mahitaji ya
kiufundi na utambuzi wa njia za kupitisha bomba na ugawaji wa kanda za
usambazaji.
Aidha alisema kuwa ili kuharakisha
usambazaji wa gesi, TPDC inakaribisha na kuhamasisha sekta binafsi
kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu itakayowezesha usambazaji wa
gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam mara tu mapitio ya upembuzi
yakinifu utakapomalizika.
Mtandao huo unakadiriwa kuwa na
urefu wa takribani kilomita 65 ambao utahudumia, kwa kuanzia, nyumba
30,000, viwanda na vituo vya kushindilia gesi asilia pamoja na vituo vya
kujazia gesi hiyo.
Katika hatua nyingine Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa hadi sasa TPDC imefanikiwa
kukiunganisha na mtandao wa gesi asilia Kiwanda kimoja cha kutengeneza
Vigae cha Goodwill kilichopo Mkuranga, Mkoani Pwani huku likiendelea na
majadiliano na viwanda vingine vitatu kwa ajili ya kuunganishwa na
mtandao huo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya
Mwaka 2015 TPDC inatambuliwa kuwa Shirika rasmi la taifa linalojiendesha
kibiashara, ambapo sheria hii inaipa mamlaka TPDC kuruhusu makampuni
mbalimbali kuendesha shughuli za sekta, zitakazokuwa zainadhibitiwa kwa
utaratibu maalum chini ya usimamizi wa Mdhibiti anayetoa leseni.
Post a Comment