Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WACHUNGAJI ZAIDI YA 300 WA MADHEHEBU MBALIMBALI KUSHIRIKI SEMINA NA KONGAMANO JIJINI ARUSHA

SAM_0052

Mch.Dr.Jerry Williamson
kutoka nchi  Marekani akiomba katika ibada ya  katika kongamano kanisa la
Zion lililopo njiro jijini Arusha ambapo kanisa hilo limeendaa semina na
kongamano  kwa wachungaji pamoja na washirika wengine,kulia kwake ni
Ben Mangeni ambaye ni mkalimani wake

 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo
Mch.George Mngodo akiongea na waandishi wa habari , alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki kongamano hilo wataweza kujifunza
mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha  kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine
Mmoja wa wachungaji wa
kanisa hilo Paul Sulley akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi
anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa  bidii.
 kushoto ni Mtume trice Shumbusho akiwa na mkalimani wake akihubiri katika kongamano  hilo
Waumini wakiwa katika maombi
Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano
 
 Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano
Picha ikionyesha madhabahuni
 Picha ikionyesha jengo la kanisa

Na Pamela Mollel,Arusha
 
Wachungaji zaidi ya 300 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini bila kujali madhehebu yao  wako katika semina maalumu ya neno la Mungu yenye
lengo la kusaidia kupeleka ujumbe wa madhihilisho ya nguvu ya kristo katika maeneo
mbalimbali ya nchi ili watu waweze kubadilika na kumjua Mungu
 
Semina hiyo ya siku nane iliyoandaliwa na kanisa la Zion City Church Arusha   litafanyika kanisani hapo   ikiambatana na Kongamano  ambalo limeandaliwa kwa ajili ya wachungaji na watu mbalimbali likiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kupeleka injili kwa watuwa mataifa.
 
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha  kuvuka kutoka hatua moja
kwenda nyingine.
 
 Mngodo aliongeza kuwa  huduma zitakazo tolewa katika katika
kongamano hilo hazitawakugusa kiroho tu bali hata kwenye maisha yao ya kawaida
wataweza kubadilika
 
“Tunaamini kongamnao
hili litagusa wachungaji hawa na jamii wanayoihudumia kimwili na kiroho”alisema
Mngodo
 
Kwa upande wake mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa  bidii.
 
Mch.Sule alisema kuwa ulimwengu wa sasa umeharibika hivyo unahitaji watumishi waliokutana na Mungu na siwanaomjua Mungu pekee ili waweze kuwatumikia watu.
 
Miongoni mwa watumishi wa Mungu wa kimataifa watakao kuwa wasemaji wakuu katika kongamano hilo ni Askofu mkuu wa kanisa la Zion City Church Arusha   John
Shumbusho pamoja na mkewe Trice Shumbusho
Wachungaji
 wengine ni kutoka nje ya nchi Mch.Dr.Jerry Williamson, Mch.Dr Jim Oxendine kutoka Marekani,Mch.Yoshua Masasu kutokaRwanda,Mch.Aloysius Kiiza kutoka Uganda,Pamoja na Mch.George Mkandawire kutoka Afrika
Kusini  .
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget