Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Muasi Bosco Ntaganda kutoa ushahidi

Bosco Ntaganda maarufu 'Terminator'Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bosco Ntaganda maarufu 'Terminator'
Aliyekua kiongozi wa waasi nchini Congo, Bosco Ntaganda anatarajiwa kutoa ushahidi leo katika mahakama ya kimatafa ya ICC.
Ntaganda aliyepewa jina la 'The Terminator ' atasimama kizimbani ikiwa ni takriban miaka miwili baada ya kesi kuanza.

Ntaganda anashutumiwa kutekeleza uhalifu na uhalifu dhidi ya binaadam unaodaiwa kutekelezwa na vikosi vyake.
Mashtaka yanasema kuwa kati ya mwaka 2002 na 2003 vikosi vyake vya uasi walivamia eneo la Ituri, wakatekeleza mauaji na vitendo vya kuwabaka raia.

Mwaka 2015, alikutwa na hatia kwa makosa 13 ya uhalifu wa kivita ikiwemo kuwasajili watoto wa umri wa chini ya miaka 15 kwenye jeshi na makosa mengine ya uhalifu dhidi ya binaadam.

Jopo lake la utetezi limepanga kuwaita mashuhuda 109 na wataalam wanne.Hii ndio sababu kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kwa miezi kadhaa.

Ikiwa atakutwa na hatia atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka 30 gerezani

CHANZO BBC NEWS
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget