Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

MANISPAA YA KINONDONI YATAKA BILIONI 4 ZILIZOPO KWENYE AKUNTI ZA KATA ZITUMIKE KWENYE MIRADI ILIYOKUSUDIWA

Mwagala


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta akizungumza wakatiwa kikao cha baraza la Madiwani katika ukumbi wa Manispa ahiyo Magomeni jijini Dar es Salaam, juni 15, 2017.

Na Humphrey Shao
Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni limeagiza kuhakikisha fedha zote zilizopo katika akaunti za kata zaidi ya Bilioni 4.9 zifanyiwe utaratibu wa manunuzi ili ziweze kutekeleza miradi iliyokusudiwa katika kata hizo.

Maazimio hayo yamefikiwa katika baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo lililongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta .


Aidha baraza hilo pia limeridhia maombi ya kamati ya Fedha kwa kutaka kubuni vyanzo vipya vya fedha vitakavyosaidia Halmashauri hiyo kupata fedha zaidi licha ya baadhi ya vyanzo kuhamia serikali kuu. 

pia kikao hicho kilipitisha azimio la kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kitendo chake cha kizalendo cha kuhakikisha kuwa fedha za watanzania zilikuwa zinapotea kutokana na mchanga wa Madini uliokuwa ukisafirishwa nje kiholela unapangiwa utaratibu wa kunufaisha Serikali.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Aron Kangurumjuli aakizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo akichangaia katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Kinondoni.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget