Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Mashehe wa Jiji la Dar es Salaam wampongeza Meya Mwita kwa kuwakutanisha waumini wa kiislam kwenye Futari jana

 Mstahiki  Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waumini wa dini ya kiislam, wananchi waliohudhuria kwenye futari hiyo Jana, mara baada ya kumaliza kufuturu.hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisalimiana na wananchi waliohudhuria kwenye hafla ya Futari jana katika viwanja vya Karimjee.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wapili kulia, akiwa kwenye meza ya pamoja na Kadhi Mkuu wa Tanzania Bara Abddallah Yusuph Mnyasi.
 Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob, akiwa pamoja na wageni waalikwa wakati wa futari ya kuelekea mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani iliyoandaliwa   na Mstahiki Meya wa jiji laDar es Salaam , Isaya Mwita jana.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam  Isaya  Mwita,
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, wananchi na wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakichukua futari kwa ajili ya kufuturu Jana.hafla hiyo iliandaliwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.

                                 Baadhi ya wageni waalikwa wageni waalikwa wakipata futari
                                   Baadhi ya wageni waalikwa wageni waalikwa wakipata futari
 Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam  Isaya  Mwita, mara baada ya kumalizika kwa futari hapo jana.
  Baadhi ya watoto yatima wakifuturu ikiwa ni moja ya futari iliyoandaliwa na mstahiki meya wa jiji la dar, isaya mwita katika kuelekea juma la mwisho la mfungo wa ramadhan karimjee dar jana
                            Sheikh wa Wilaya ya Ilala Adam Mwinyipingu akitoa neno la shukurani

  NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita jana aliwafuturisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam zaidi ya 600
 kutoka sehemu mbalimbali  jijini hapa nakutumia nafasi hiyo kuwatakia waumini wote wa dini ya kiislam heri ya kumalizia Ibada ya Kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani sambamba na kuingia kwenye sikukuu ya Idd.

Aidha Mashehe wa jiji la Dar es Salaam waliohudhuria Futari hiyo jana walimpongeza Meya Mwita kwa kuandaa Futari hiyo na kusema kuwa ni jambo la heri kwao na hivyo wataendelea kumuunga mkono katika shughuli zake za kuwaongoza wananchi kwa ajili ya kuwaletea Maendeleo.

 Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na Kadhi Mkuu  wa mkoa , Mashehe wa jiji la Dar es Salaam, viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, makundi mbalimbali ya kijamii,  ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini hapa.

 Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa  Futari hiyo jana Meya  Mwita alisema kuwa kupitia  mfungo wa Ramadhani  wakazi wa jiji na watanzania wote kwa ujumla wanapaswa kuzidisha hali ya unyenyekevu, ucha mungu ili kutenda mambo yaliyomema na hivyo kusherehekea sikukuu ya Idd kwa hali ya utulivu.

Meya Mwita alifafanua kuwa kupitia hafla hiyo imekuwa ni fursa ya kipekee kujumuika pamoja na wananchi wa jijini hapa kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo na kutumia nafasi hiyo kuwaalika kwenye ofisi za jiji hilo ili aweze kusikiliza kero zinazo wakabili na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

“Nimefarijika sana leo, kujumuika pamoja kwenye tukio hili muhimu ambalo hutokea kila mwaka , lengo la kuwa na hafla hili , ni kuungana na waumini wote wa dini ya  Kiislam wa jijjni hapa ambao wako katika mwezi mtukufu wa Ramadhani "

"Lakini pia hata wale ambao hawapo kwenye mfungo huu,  kupitia hadhara  hii tunaweza kukutana na wakazi wengi zaidi na kubadilishana mawazo”.alisema Meya Mwita.

Jiji hili ,lina wakazi wengi sana, ambapo huwezi kusema kwamba leo utakwenda kukaa na kila mmoja , lakini yapo matukio ambayo yanatukutanisha kama wanafamilia wa jiji la Dar es  Salaam , na hii kwangu ndio faraja zaidi, kutokana tunakutana kwenye matukio ya kiimani, nasio ya kisiasa.


Kwa upande wake  Sheikh wa Wilaya ya Ilala Adam Mwinyipingu alimpongeza Meya Mwita kwa kuandaa hafla hiyo iliyomkutanisha na baadhi ya wananchi ambao walishiriki futari hiyo.


Sheikhe Mwinyipingu alisema kuwa  jambo hilo ni la heri kwa waumini wote wa kiislam na wananchi wote waliohudhuria Hafla hiyo ya futari.

Kwa upande wake  Mbunge wa Jimbo la  Temeke, Abdallah Mtolea pamoja na mambo mengine alimpongeza meya Mwita kwa kuandaa hafla hiyo, na kusema kuwa imesaidia kuwakutanisha na wananchi wao ambao si rahisi kukutana nao mara kwa mara  kutokana
na shughuli zao.

“ Kwa siku ya leo nimeifurahia nimeweza kujumuika na viongozi mbalimbali wa dini, vyama vya kisiasa, na wananchi wa jiji hii ambao tunashindwa kukutana mara kwa mara kutokana na shughuli mbalimbali ambazo wametupatia wananchi ili kuwatumikia.

Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget