Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

UPATIKANAJI WA DAWA KWENYE VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA WAFIKIA ASILIMIA 80

MWAGALA

 Mganga Mkuu wa Jiji la
Tanga(CMO), Jairy Khanga akifungua mafunzo ya  mradi wa tumaini la mama
uliyowahusisha wauguzi kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini
ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya Mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri
mjini Tanga kulia ni Msimamizi wa Mfuko huo,Dina Mlwilo kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga
Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Mkoani Tanga (NHIF) Dinna
Mlwilo akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga wakati wa mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha
wauguzi kutoka halmashauri za
Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga
uliofanyika mjini hapa  ambapo
alisema asilimia 70 wakina mama wajawazito wamejiunga na mradi wa tumaini la mama kwa ajili ya kupata
matibabu
 Mwezeshaji wa mafunzo wa
Tumaini la Mama,Ally Omari
akisisitiza jambo wakati 
akitoa somo kwenye
mafunzo hayo



Mmoja wa wasimamizi wa mradi wa Tumaini la Mama Tanzania
Irine Meaki akielezea masuala mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa halmashauri ya Jiji.
 
 
 Baadhi ya wauguzi
wanaohudumia wakina anama wajawazito
wakimsikiliza mgeni rasmi
wakati alipofungua mafunzo ya mradi wa
tumaini la mama uliyowahusisha
wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga
chini ya usimamizi wa mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.
Baadhi ya washiriki
wakifuatilia mafunzo
wakati wa mafunzo ya
mradi wa tumaini la mama
uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito
kutoka halmashauri za Tanga
Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani
Tanga.


Baadhi ya washiriki
wakifuatilia mafunzo
wakati wa mafunzo ya
mradi wa tumaini la mama
uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito
kutoka halmashauri za Tanga
Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.
 Msimamizi wa Mfuko
huo,Dina Mlwilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo hayo
UPATIKANAJI wa dawa kwenye
vituo vya Afya kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga umeelezwa kufikia asilimia 80 kwa wagonjwa
wanao kwenda kupata matibabu
wakiwemo wanaohudumiwa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Hayo yalibainishwa na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga(CMO), Jairy Khanga wakati alipofungua mafunzo
ya mradi wa tumaini la mama
uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito
kutoka halmashauri za Tanga
Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga. Alisema upatikanaji huo wa dawa umesaidia kuweza kuwadumia wakina
mama wajawazito ambao wamekuwa
wakijitokeza kupata huduma za matibabu na vifaa tiba pamoja na wategemezi wao.
Aidha alisema jambo hilo limeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa
kupunguza na kuondokana na
vifo vya wakina mama wajawazito ambavyo vilikuwa vikijitokeze kutokana na kukosa
huduma muhimu za matibabu wakati
wanapojifungua.
Alisema kutokana na umuhimu wa mradi huo watoa huduma wanapaswa
kuweka mipango mizuri ya
kuwahudumia wakina mama wajawazito wakati wanapofika kwenye vituo vyao vya afya ili
waweze kuepukana na athari zinazoweza
kujitokeza kutokana na hali walizokuwa nazo.
“Mradi huu una zaidi ya miaka minne nyie kama watoa huduma
mnauzoefu mkubwa hivyo kupitia
mafunzo hayo jaribuni kushirikiana na wawezeshaji kuhusu changamoto zinazowakabili
wakati wa utekelezaji wake “Alisema.
Aidha pia aliwataka watoa huduma wafanye uhamasishaji mkubwa kwa wakina mama wajawazito waliopo
kwenye maeneo yao kwa lengo la kuongeza wigo mpana wa kuwaandikisha kwenye mradi huo ambao ni
muhimu kwao.
Akichangia wakati wa uwasilishwaji wa mada mbalimbali katika
mafunzo hayo,Mratibu wa Mfuko
wa Afya ya Jamii (CHF) wilayani Mkinga Elizaberth Dickson alisema moja kati ya changamoto
kubwa zilizopo hivi sasa ni
ucheleweshwaji wa kadi za bima ya afya kwa wakina mama wajawazito jambo ambalo
linakwamisha huduma kwa baadhi yao
wanapohitaji
matibabu.
“Lakini nisema upatikanaji wa kadi za mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
kwa wakina mama wajawazito na
wategemezi kwa wakati zitarahisisha
upatinaji wa huduma za matibabu katika vituo mbalimbali vya
afya ndani na nje ya
mkoa”Alisema
Katika kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wakina mama wengi
mkoani Tanga, Msimamizi wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo aliwataka watoa huduma
kuihamasisha jamii kuona umuhimu
wa kuajiandikisha katika vituo vya afya wakati wa ujauzito
kupitia mradi huo
“Kwani kujiandikisha huko wanaweza kupata fursa muhimu ya kupitia mradi wa tumaini la mama kwa kupata
huduma za matibabu wao na
wategemezi wao kwenye vituo vya afya “Alisema.
Aidha alisema kwa mkoa wa Tanga tayari wamekwisha kuandikisha
wakina mama wajawazito
asilimia 70 ambao wananufaika kupitia mpango huo ambao una lengo la kupambana na vifo
wakati wanapojifungua.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget