Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WCF YATOA MUONGOZO WA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI KWA MADAKTARI


Mwenyekiti
wa bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Emmanuel
Humba, akifungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari 70 kutoka hospitali 35 za
umma na binafsi jijini Dar es Salaam kuhusu namna  ya kufanya tathmini ya
ugonjwa na ajali, kabla ya kumlipa fidia mfanyakazi aliyeathirika. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba na katikati ni
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar


Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba,
(aliyesimama),akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa
madaktari kuhusu namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali apatayo
Mfanyakazi mahala pa kazi ili taratibu za fidiwa zifanyike. Mafunzo hayo
yaliyowaleta madaktari 70 kutoka hospitali 35 za umma na binafsi za jijini Dar
es Salaam, yameanza leo Juni 19, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, na katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar



NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umetoa muongozo utakaotumiwa na madaktari na
watoa huduma za afya, wakati wa kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa
mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi.
Muongozo
huo ni miongoni mwa masuala mbalimbali watakayojifunza madaktari wapatao 70
kutoka hospitali 35 za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo,
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw  Masha
Mshomba, alisema kuwa  madaktari ni wadau
muhimu sana  katika kufanikisha shughuli
za Mfuko huo.
“Tunataka
hawa  madaktari wawe na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha
kufanikisha azma yetu, na tumeamua kuwa mafunzo ya aina hii yatakuwa endelevu
ikiwa ni pamoja na kuwapatia muongozo utakaowasaidia kutekeleza majukumu yao ya
kufanya tathmini,” alisema.
Alisema
kuwa katika jitihada za kuendeleza mafunzo hayo, Mfuko huo una mpango wa
kushirikiana na vyuo vikuu nchini katika kutoa huduma hiyo.
Kuhusu
wafanyakazi walioripoti matukio ya ajali kazini
kwenye Mfuko huo hadi hivi sasa, alisema jumla ya kesi 670 za wafanyaakzi
walioumia na kuhitaji matibabu zimepokelewa.
Alisema
kuwa  wengi wa wafanyakazi waliopatwa na
matatizo hayo kazini wanatoka sekta mbali mbali kama migodi, viwanda na
usafirishaji. Aliwaomba wafanyakazi walioumia wakiwa kazini kuwasiliana na Mfuko
huo ili kuweza kusaidiwa.
Alibainisha
kuwa Mfuko umeingia mkataba na watoa huduma za afya kwenye hospitali na  vituo vya
afya  zaidi ya 6,000 nchi nzima
ambapo zitahudumia wafanyakazi hao.
Alisema
huduma za matibabu zinatolewa kwa mfanyakazi atakayeumia au kuugua kutokana na
kazi. Huduma hizo ni ya gari la kubeba wagonjwa, kumuona daktari,upasuaji,
uuguzi, dawa, kurudia matibabu itapobidi na kupatiwa viungo bandia.
Alibainisha
kuwa wajibu wa mfanyakazi ni pamoja na kuifahamu sheria ya fidia kwa wafanyakazi,
(sura 263 marejeo ya mwaka 2015), kutoa taarifa kwa wakati kwa mwajiri au
Mkurugenzi Mkuu pindi atakapopatwa na ajali kazini au kubainika kuwa na
magonjwa yanayotokana na kazi.
Aliwaomba
wafanyakazi hao kutoa ushirikiano pindi wanapotakiwa kufanyiwa uchunguzi wa
matibabu, kuzingatia maelekezo yatolewayo na Mamlaka mbali mbali  kuhusu usalama mahali pa kazi, kuzingatia
sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbali mbali kuhusu masuala ya fidia kwa
wafanyakazi , kutunza kumbukumbu binafsi zinazohusu masuala ya kazi.
Akifungua
mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba
aliwashauri madktari hao kufanya kazi zao kwa weledi zaidi ili kuongeza tija na
ufanisi kwa lengo la kuiwezesha sekta hiyo kuongeza wigo wa upana wa  huduma.
Bw.
Humba alisema kuwa  azma ya mfuko huo
kuwa na mtandao mkubwa wa watoa huduma za afya nchi nzima ambao watasaidia
Mfuko kutoa fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyepata maradhi au majeraha wakati
akitekeleza wajibu wake kazini.
“Nyie
ni wadau muhimu sana katika kutuwezesha sisi kufanya kazi zetu vizuri
ninawaombeni  mzingatie yote
mtakayofundishwa kwenye mafunzo haya  na
kuongeza weledi  wenu ,” alisema.
Alisema
kuwa watoa huduma hao ndio tegemeo kubwa la kupata taarifa sahihi za mgonjwa
pindi anapopata matatizo akiwa kazini, kwani
ndipo utaratibu wa malipo au fidia unapoanzia.
“Lazima
mjue kuwa pakitokea tatizo lolote la mfanyakazi kulipwa fidia tutanzia kwenu
ili kutupa taarifa sahihi kuhusu wagonjwa wa aina hiyo,” alifafanua.
Aidha
Bw Humba aliwataka madaktari hao kusaidia kuwaelimisha wateja wao juu ya huduma
mbali mbali zinazotolewa na mfuko huo.
“Mara
nyingine unaweza kukutana na mgonjwa akakuuliza kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko
huu, ndio maana tumewaita hapa kuwaelezeni
yote, tunaomba mtusaidie kuwaelimisha,” alisisitiza.
Mwenyekiti
huyo, aliutaka uongozi wa Mfuko  huo
kuangalia namna ya kuyafanya mafunzo hayo kuwa endelevu .
“Ninashauri
uongozi wa mfuko kuwa na mafunzo
endelevu ya aina hii, ili kuwakumbushia watoa huduma wetu  waweze kuendena na wakati,” alisema.
Alidokeza
kuwa  hadi sasa Mfuko umekwisha endesha
mafunzo ya aina hiyo sehemu mbali mbali nchini na kushirikisha madaktari
wapatao 359.
“Tulianza  kutoa mafunzo ya aina hii mwaka 2015 ambapo
tumewashirikisha madaktari kutoka  Kanda
ya Mashariki, Ziwa, Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini,”alisema

 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza kwenye mafunzo hayo
 Sehemu ya madaktari wanaohudhuria semina hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto) akiteta jambo na Daktari Bingwa wa upasuaji na majeruhi wa Taasisi ya Mifupa MOI, Dkt. Robert Mhina
 Dkt. Daniel Estomiah Kimaro, kutoka hospitali ya Bochi akizunguzma kwenye mafunzo hayo
 Mtaalamu mbobezi wa masuala ya afya na kazi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili jijini Dar es Salaam, (MUHAS), Yahya Kishashu, (kushoto), na Daktari bingwa wa upasuaji na majeruhi, kutoka MOI, Dkt.Robert Mhina, wakiwasilisha mada juu ya magonjwa yatokanayo na kazi pamoja na ajali mahala pa kazi.
 Bw. Masha akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw.Anselim Peter, Mkuu wa Kitengo mcha Sheria cha Mfuko, Bw. Abraham Siyovelwa, na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Bi. Laura George, wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko ya chai.
 Afisa Uhusiano wa WCF, Bi. Zaria Mmanga, akigawa taarifa mbalimbali zihusuzo mafunzo hayo
 Meneja Madai wa WCF, Bi. Rehema Kabongo, (katikati), akizungumza jambo na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Bi. Laura George, (kulia) na kushoto ni Afisa Uhusiano wa WCF, Bi. Zaria Mmanga


 Maafisa wa juu wa WCF, bw. Stephen Goyayi, (Kushoto) na Bw. james Tenga, wakiwa kwenye mafunzo hayo

Picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi na uongozi wa WCF
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget