Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Trump anatumia nafasi yake kujinufaisha?

  •         

Rais Donald Trump anashutumiwa kutumia nafasi ya urais kujipatia faida zaidiHaki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Donald Trump anashutumiwa kutumia nafasi ya urais kujipatia faida zaidi
Takriban wanachama 200 wa Democrats katika Bunge la Congress wameunganisha nguvu ili kufungua kesi dhidi ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuhusu nyaraka za malipo kutoka serikali za nje kupitia biashara zake.
Trump anashutumiwa kukiuka kipengele cha katiba kuhusu malipo, kinachopiga marufuku kujipatia faida au fedha bila bunge kupitisha.

Hata hivyo wanachama hao wamesema idadi hii ni kubwa kuwahi kutokea kutaka kumshtaki Rais wa Marekani.
Maafisa wa Serikali na wafanyabiashara binafsi pia wanamfungulia mashtaka rais Trump kwa madai hayo hayo.

Aidha Ikulu ya Marekani imekana madai hayo ambapo Idara ya Sheria imekataa kuzungumzia madai hayo ya wabunge, lakini awali ilisema ni kinyume cha katiba kumshtaki Rais kama mtu binafsi.

Wabunge wamedai kuwa Trump hakutaka idhinisho la Congress kwa malipo yoyote yaliyopokelewa katika biashara zake Kutoka serikali za nje tangu alipoingia madarakani.

''Rais Trump ana mgongano wa maslahi katika nchi takriban 25, na inaonekana anatumia nafasi yake kujiongezea faida'' alieleza John Conyers, akinukuliwa na shirika la habari la Uingereza, Reuters.

CHANZO BBC NEWS
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget