Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

RC MASENZA AFUTULISHA ZAIDI YA WATU MIA MBILI (200)

 
 Mkuu wa mkoa wa Iringa bi Amina Masenza akiwa sambamba na katibu tawala wa mkoa wa Iringa bi wamoja Ayoub wakiwa katika viwanja vya Ikulu ndogo wakifurahia jambo baada ya futari ya pamoja wa watu zaidi ya miambili
Baadhi ya watu waliojitokeza kushiriki futari pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza.
 
Na Fredy Mgunda, Iringa
 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina masenza amefutulisha futari  watu zaidi ya mia mbili katika eneo la Ikulu iliyopo kata ya gangilongo kwa lengo kudumisha amani na upendo.
 
Akizungumza baada ya futari Mkuu wa mkoa masenza aliwataka waumini wote wa dini ya kiislamu na wakristo kuwa makini katika maeneo ya ibada ili kuepukana na kutoka kwa shambilio lolote lile ambalo litasababisha maafa.
 
“Tumeona nchi nyingine kipindi hiki cha ramadhan kukitokea milipiko mingi ya kujitoa mhanga kwa baadhi ya watu wenye itikadi kali hivyo tunapaswa kuwa makini mno mwezi huu hata miezi mengine yote kwa kudumisha amani yetu”alisema Masenza
 
Masenza aliwaomba wananchi wote wa mkoa wa Iringa kuwafichua waalifu wanaofanya shughuli hiyo kwa njia yoyote ile ili kuendelea kudumisha tunu tuliyokuwa nayo toka wakati tunapata Uhuru hadi hii Leo.
 
Aidha Masenza aliwaomba watanzania kuendelea kumuunga mkono na kuombea Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli katika vita hii ya kukuza uchumi kutoka hapa tulipo hadi uchumi wa kati kwa kuwa vita hii sio lelemama.
 
“Ni kitu kigumu sana unapogusa maslai ya mtu binafsi kwa maslai ya wanyonge huwa inakuwa vita kubwa kupambana nayo lakini Rais wetu mpendwa anafanikiwa hilo hivyo lazima tuwe tunamuombe na kumuunga mkono ili tuendelee kumpa moyo kwenye vita hii” alisema Masenza
 
Niwaombe wananchi wa mkoa wa Iringa kuwapuuza viongozi wanaopotosha ukweli wa mambo ambayo serikali inayafanya kwa manufaa ya wananchi wa kipato cha chini,kati na wale wenye kipato kikubwa pasipo kumnyang’a au kumdhulumu mtu haki yake.
 
Katika futari hiyo kulihudhuriwa na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Iringa kama Kilolo iliwakilishwa na mh Asia Abdalah,Mufindi Jamhuri William na wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
 
Lakini mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliwataka wananchi na viongozi kutunza amani na kuacha kufanya uharifu kipindi hiki cha ramdhan hata baada ya kuisha ramadhan ili kuendelea kuweka nchi kwenye utulivu uliopo sasa.
 
“Unakutana na mtu kipindi hiki anajifanya kafunga lakini matendo yake hayaendani ya wakati uliopo lakini kuna wengine saizi wametulia ila ramadhan ikiisha tu anaanza matendo ya uvunjifu wa amani hivyo niwaombe tena na tena wananchi kutunza amani iliyopo “alisema Abdalah
 
Abdalah alimshukuru mkuu wa mkoa wa Iringa bi Amina masenza kwa futari ambayo imewakutanisha watu mbalimbali kukaa pamoja na kubadilisha mawazo japo kwa muda mchache hivyo kuwaomba wakuu wenzake wa wilaya zote za mkoa wa Iringa kuiga mfano wa mkuu wa mkoa.
 
Nao baadhi ya viongozi wa dini waliofika eneo la futari walimpongeza mkuu wa mkoa kwa kufutulisha watu mbalimbali ambao imekuwa fursa ya kufanya wabadilishane mawazo ya kujenga tofauti na kila mmoja angefuturu kwake.
 
“Hili ni jambo jema sana kwa kiongozi wetu wa mkoa maana leo tumekutana na viongozi kutoka dini mbalimbali hata wengine sio viongozi lakini tumebadishana mawazo na hili ni jambo jema kwetu sisi kwa ukweli tumejifunza mambo mengi leo mungu ambariki mheshimiwa mkuu wa mkoa” walisema viongozi wa dini
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget