Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Meya wa jiji la DSM Mwita awashukia madereva wanaosafirisha wanafunzi wanaosoma shule zilizopo katikati ya jiji






MWAGALA
 Guest of honor   Lord Mayor  of Dar es salaam city Isaya Mwita  delivering  a speech   during  a commemorating the UN road safety week today at Upanga  Dar es salaam  

 President of AAT  Nizar jivan  welcomming the Guest of honr  Lord  Mayor of Dar  es salaam Isaya Mwita and invited Guest   to  be   part of  function   in innaguration   of road signs set  near school zone    by AAT to save lives of Young children  at Shaban Robert Road Upanga today.



Director  and CEO of  AAT Mr Yusuf Ghor speeking to Invited Guest during  the function of  the program of installing appropriate   road signs  near the schools to  save  the lives of  students . 


 Mayor of Dar es salaam Isaya Mwita  during  the function of  the program

 President of AAT Nizar  Jivan   giving a gift to guest of honor Lord Mayar of Dar es salaam Isaya Mwita  to apreciate  his support  toward  the  initiative of saving lives  of  young children and all road users.


 Lord Mayor  of Dar es salaam city Isaya  Mwita  innagurating one of road signs set by AAT   during   the program  of installing road signs near   the schools Shaban Robert Road Upanga Dar es salaam.


 Students from  Olympio and   Diamond Primary  school  partcipating in the function of  innagulation of  the  road signs  near their schools  set by AAT and FIA   .

  The group photo of  pacitpants  including  Students from  Olympio and   Diamond Primary  school during  the function of  innagulation of  the  road signs  near their schools  set by AAT and FIA   .

 Miss Tanzania Diana Edward   adressing the audience  during the function  hosts by AAT and FIA  to save lives of  Young  children  today.

Some of road users including students  given some knowledge of using  zebra closing by Mr Kombo  as a public relation officer of AAT



NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka madereva wanaowasafirisha wanafunzi wanaosoma  shule nilizopo katikati ya jiji kuwashusha na kuwachukua  ndani  ya kuta za shule badala ya kuwashusha  na kuwachukua nje.

Meya Mwita aliyasema hayo jijini hapa leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya Kimataifa ya usalama barabarani ,ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa utaratibu wanaoutumia madereva hao ni hatari kwa wanafunzi  kwani inawalazimu  kuvuka barabara.

Alisisitiza kuwa iwapo watatumia utaratibu wa kushusha wanafunzi ndani ya kuta za shule itasaidia kupunguza hatari kwa wanafunzi ikiwemo kugongwa na gari, pikipiki, kupunguza msongamano wa magari barabarani.

" Jambo ambalo linakwenda kufanyika leo ni muhimu sana, limesaidia kuongeza usalama wa watoto wetu ambao wanasoma kwenye shule hizi zilizopo katikati ya jiji, lakini pia linatoa nafasi kwa walimu kuwa na uhakika wa usalama wa  wanafunzi wao, najua wakati mwingine mmekuwa na wasiwasi kuhusu usalama wao.

" Nipende kutoa rai kwa madereva, zingatieni jambo hili , mabasi ya shule yawe yanachukua na kushusha wanafunzi ndani ya kuta za shule , utaratibu ambao mlikuwa mnautumia hivi sasa usitishwe mara moja.

Huko ni kuhatarisha maisha ya wanafunzi , ambao badae wangekuwa madokta , wabunge, marais , ndio ambao tunawategemea , watoto ndio Taifa la kesho, nawaomba sawa , walimu mlisimamie jambo hilo,

Aidha Meya Mwita aliwataka walimu na shule kwa ujumla kutumia kwa umakini vifaa vya usalama barabarani katika mitaala ya shule ili kuwafundishia wanafunzi masuala ya usalama barabarani kwani kutafanya watambue elimu hiyo na hivyo kuleta manufaa kwa Taifa.

Alisisitiza kuwa " elimu hii ikifundishwa vizuri itapunguza ajali za barabarani wakati wa kuvuka lakini pia hata pikipiki zitaendeshwa kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ,bila kuathiri watumiaji wengine wa barabara.

Hata hivyo Meya Mwita aliwapongeza Automobile Association Of Tanzania (AAT), na Federation International Automobile (FIA) kwa kuchukua jukumu la kupunguza ajali barabarani na kuokoa maisha ya wanafunzi.

AIdha AAT, FIA  kwa kushirikiana na kitengo cha Usalama barabarani elimu kwa umma, wamefundisha walimu 1000 kutoka shule 51 za jiji la Dar es Salaam kuhusu matumizi sahihi ya alama za barabarani na matumizi sahihi ya  barabara ambapo matarajio yake ni kuwafikia wanafunzi wengizaidi.

Sambamba na hilo , AAT, FIA imeahidi kutoa elimu hiyo kwa kila halmashuri za jiji la Dar es Salaam ambapo jumla ya watu 10 watakuwa wakipatiwa mafunzo hayo.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget