Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Mataifa 4 ya kiarabu yaipa Qatar masharti 13 kuafikia la sivyo itengwe

Saudia imefunga mpaka wake wa ardhini kati yake na QatarHaki miliki ya pichaAFP
Image captionSaudia imefunga mpaka wake wa ardhini kati yake na Qatar
MATAIFA manne ya kiarabu yameitumia Qatar masharti 13 ambayo ni sharti iafikie iwapo inataka kuondolewa vikwazo kulingana na vyombo vya habari.
Saudia, Misri, UAE na Bahrain zinataka taifa hilo kufunga kitu chake cha habari cha Aljazeera.
Pia wanaitaka Qatar kupunguza ushirikiano na Iran na kufunga kambi moja ya wanajeshi ya Uturuki katika kipindi cha siku 10 pekee.
Qatar imekana kufadhili magaidi hatua inayosababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.
Taifa hilo limekabiliwa na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa kipindi cha wiki mbili ikiwa ni mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa kati ya mataifa hayo ya Ghuba kwa miongo kadhaa.
Ramani ya majirani wa taifa la Qatar
Image captionRamani ya majirani wa taifa la Qatar
Orodha hiyo ilitangazwa baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson kuwaambia majirani wa Qatar ''kuweka mahitaji yao na kuchukua hatua''.
Waandishi wanasema kuwa Marekani ambayo inataka kutatua mzozo huo imekuwa na matatizo, kuhusu kipindi cha Saudia na mataifa mengine kuweka rasmi mahitaji yao.
Hakujakuwa na majibu ya moja kwa moja kutoka Qatar lakini waziri wa maswala ya kigeni Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani alisema awali kwamba Qatar haitafanya majadiliano yoyote hadi pale vikwazo hivyo vitakapoondolewa.
CHANZO BBC NEWS
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget